Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt .Philip Isdor Mpango
ameshtushwa kupata fununu ya baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi,
kuhusika kuwa vinara wa kuchochea wananchi kuhujumu miundombinu ya
miradi ya kimkakati ikiwemo reli ya kisasa (SGR) pamoja na kupora ardhi
za wanyonge.
Aidha
ameziagiza kamati za siasa kuanza kubaini kambi na makundi ambayo
yameanza kujitokeza kuanza kampeni za chinichini kuelekea katika
uchaguzi wa ndani wa CCM mwaka 2022.
Pamoja na hilo ,Mpango amehimiza, wananchi kujitokeza katika zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwakani .
Akizungumza
na madiwani,wabunge na kamati za siasa Wilaya na mkoa mkoani Pwani
,alisema pamoja na mafanikio yaliyopo Pwani amebaini changamoto sita
ambazo zinahitaji ufumbuzi ili kupata ushindi mzuri uchaguzi mkuu ujao
2025.
Mpango
alieleza ,kubwa ni kuhujumu miradi ya kitaifa ya kimkakati ikiwemo
mradi mkubwa wa umeme (Stigo )Rufiji na reli ya kisasa (SGR) ambapo
baadhi ya wananchi wakichochewa na viongozi wa CCM .
"Upo wizi wa saruji pale mradi wa umeme Rufiji na kwenda kuuza Kwingine vitendo hivi havikubaliki na havivumiliki "
Pamoja na hilo, kusheheni kwa migogoro ya ardhi inayohusisha baadhi ya viongozi wa CCM na watumishi wa ardhi kupora maeneo.
"Nimesikitishwa kusikia wapo wanaohusika kupokonya haki za wanyonge,naagiza hili lisimamiwe na likomeshwe ibaki historia "
Mpango
aliipongeza Mkuu wa mkoa wa Pwani, Aboubakari Kunenge kwa kusimamia
changamoto hizo na kukaza kamba kwa hayo ,hivyo ameviagiza vyombo vya
dola na taasisi husika kupeana taarifa linapotokea tukio na kuimarisha
ulinzi wa miundombinu.
"Miradi
hii inatekelezwa kwa jasho la watanzania kwahiyo vyombo vya dola
viimarishe ulinzi na kuchukua hatua kali za kisheria pale wanapobaini
wahusika"
"WanaCCM
mzingatie msingi wa maadili,ibara ya 113-116 ya ilani ya utekelezaji ya
CCM imeweka msisitizo wa kupambana na rushwa ,Msiwe sehemu ya hii
dhuluma ,tutanyimwa kura "alifafanua Mpango.
Akitaja
changamoto nyingine ni za kiuchumi ,amewataka kuibua vyanzo vipya vya
mapato na kuagiza miradi na raslimali iliyopo kuilinda .
Katika
hili aliagiza kuona thamani ya fedha kwenye ujenzi wa jengo la CCM
mkoa ambalo limechukua muda mrefu na mjenzi kutimiza kazi yake.
Mpango
alitaja na changamoto ya kadi za kielektroniki na ametoa hofu kuwa
hatua zinachukuliwa na wakati wowote tatizo hili linakwisha.
Akizungumza
kuhusiana na fursa za vijana Pwani ,ili kujiimarisha kiuchumi alitoa
rai kwa vijana kuchangamkia fursa zilizopo ukizingatia mkoa huo una
viwanda vingi .
Wakati
huo huo ,Mpango alipongeza kumalizwa kwa mvutano ndani ya kamati ya
siasa mkoani Pwani na kudai hataki na hatopenda kusikia moshi unafukuta
Tena .
Aliwasihi
madiwani na wabunge kushirikiana na kuagiza wabunge na madiwani ratiba
zao za ziara kuhakikisha wanapelekea nakala kamati ya siasa na mkoa.
Mpango
hakusita kupokea changamoto zilizotolewa na Mwenyekiti wa CCM Pwani
Ramadhani Maneno kuhusu kufungua baadhi ya barabara muhimu ikiwemo
Mkuranga, Rufiji-
Mloka ,Makofia- Mlandizi na kutatua tatizo la Bandari ya Bagamoyo.
Awali
Maneno aliipongeza serikali kwa hatua ilipofikia mradi wa daraja jipya
la kisasa WAMI ambalo linakwenda kufungua milango ya kiuchumi.
Maneno
aliipongeza Serikali kwa utekelezaji wa ilani hasa kwenye miradi ya
kimkakati na fedha zilizotokana na miamala ya tozo kutumika vizuri na
faida yake kuonekana .
Nae
MNEC Pwani,Hajji Jumaa aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa
kupunguza wigo wa kundi la wenye ulemavu kukopesheka kutoka watano hadi
mmoja ambae anaweza kukopesheka kupitia asilimia 10 kwenye Halmashauri.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, Aboubakari Kunenge alisema wamepokea maagizo yote na watayafanyia kazi .
Alisema dhamana waliyopewa ni kutumikia wananchi na kuiahidi serikali kutoiangusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...