Na Samwel Mtuwa - Dodoma.

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzani(GST) imeshauriwa kufanya Utafiti wa jiosayansi katika viwanja mbalimbali ikiwa pamoja na viwanja vinavyotarajiwa kwa ujenzi wa majengo marefu ya taasisi binafsi na mashirika ya Umma kwa lengo la kufanya ujenzi uliobora kwa makazi pamoja na  miundombinu.

Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 12,2021 na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Kaspar Mmuya alipotembelea banda la GST lililopo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dodoma.

Mapema alipofika katika banda hilo alipokelewa na wataalam wa GST na kuelezewa juu kazi mbalimbali za kitaalam zilizofanywa na GST katika Majanga ya asili ya jiolojia kama vile Mipasuko ya Ardhi, kububujika kwa tope, kudidimia kwa Ardhi, pamoja na Matetemeko ya Ardhi ambapo kazi zote zilizofanyika zimeleta matokeo chanya katika Kupunguza Majanga ya asili ya jiolojia ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa Umma juu ya namna gani wanaweza kujizuia kabla , wakati na baada ya janga husika la Jiolojia.

Baada ya kupata maelezo husika juu ya Majanga ya asili ya kijiolojia , Naibu Katibu alishauri kuwa elimu ya namna hii iendelee kutolewa hata baada ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa ambayo kilele chake kitakuwa oktoba 13 , 2021 ambapo kitaifa ifanyikia Chato.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Menejimenti ya  Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Luteni Kanali Selestine Masalamado alitoa wito wa mshikamano baina ya serikali na taasisi zake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta binafsi  zinazojishughulisha na Majanga ya asili hususani katika kutoa elimu endelevu kwa jamii kwasababu kwa kufanya hivyo itasaidia kuiokoa jamii na Mali zao pale Majanga yanapokea.

"Moja ya njia za kupambana na Majanga ya asili ambayo ndio yanaleta Maafa ni kushirikiana kwa kujumuisha utaalam wa kila Idara husika kwa Umoja huo tunaweza kuikoa Dunia" alisema Kanali Masalamado.

Mpango wa kutekeleza mikakati yakupunguza madhara ya Maafa sambamba na maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi ni lengo la sita (f) la mkakati wa Sendai.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Kaspar Mmuya (aliyevaa Suti) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wataalamu wa GST katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dodoma.

Mtaalam wa GST, Batwenge Chakutema akimuelezea mdau jinsi GST inavyoshughulika na Majanga ya asili ya jiolojia , katika Banda la GST lililopo Viwanja vya Nyerere Square ikiwa sehemu ya kuekea kilele cha ushiriki wa Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...