Ukuaji wa uchumi robo ya pili mwaka 2021, KATIKA kipindi cha robo ya pili (Aprili - Juni) mwaka 2021 umeongezeka kwa kiwango cha asilimia 4.3 ikiwa ni pointi za asilimia 0.3 zaidi ya ilivyokuwa katika robo ya pili ya mwaka 2020.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Daniel Masolwa amesema katika kipindi Kama hicho mwaka 2020 aidha pato halisi la Taifa liliongezeka hadi shilingi trilioni 33.4 mwaka 2021 kutoka shilingi 32.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2020 uchumi ukiongezeka kwa kasi ndogo  zaidi ya asilimia 4.0 tangu mwaka 2017 kulikosababishwa na adhari za janga la UVIKO-19 baada ya nchi nyingi  kuzuia wananchi wake kusafiri nje ya nchi ili kudhibiti kuenea kwa UGONJWA huo.hatua hizo ziliathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii.

Hata hivyo Masolwa amesema katika kipindi cha robo ya mwaka 2021 shughuli ya habari na mawasiliano ukiongezeka iliongezeka  kwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa asilimia 12.3 ikifuatiwa na uzakishaji wa umeme (asilimia 12.1) huduma zingine za jamii zikijumuisha sanaa na burudani  na shughuli za kaya katika kuajiri (asilimia 10.8)  malazi na huduma za chakula (asilimia 10.1)
Usambazaji maji (asilimia 8.4) na uchimbaji wa Madini na mawe (asilimia 7.3).


Katika hatua nyingine Msolwa ametoa ufafanuzi was Mikoa Tajiri na Masikini ambapo amesema uchambuzi na usambazaji vwa takwimu  mbalimbali unahitaji weledi ili kutoa  taarifa sahihi kwa jamii.
" Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazoainisha mikoa tajiri na maskini hapa nchini ingawa Takwimu hizi zimetokana na chanzo sahihi lakini tafsiri yake inapotosha kwa kikasi kikubwa hivyo ofisi ya Taifa ya Takwimu hapa nchini Ina wajibu wa kutoa tafsiri sahihi ya Takwimu mbalimbali" Msolwa.

Uchambuzi wa kuabini Mikoa Masikini na  tajiri unatakiwa utumie kiashiria zaidi ya pato la Taifa viashiria vingine vinaweza kuzingatiwa ni pamoja na mfumuko wa bei, kiwango cha elimu, afya, maji, miundimbinu ya usafiri na masoko akimakiza Daniel Masolwa katika taarifa yake hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...