Na John Walter-Babati

Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Paulina Gekul leo jumanne oktoba 12, 2021 amefunga mafunzo ya mchezo wa Netiboli yaliyokuwa yakisimamiwa na chama cha Mpira wa Netiboli Tanzania (CHANETA) katika Uwanja wa Kwaraa Mjini Babati.

Mafunzo hayo ambayo yamehitimishwa rasmi leo yalilenga kuwaandaa Waamuzi wa mchezo wa netiboli katika ngazi zote.

Jumla ya washiriki 35 kutoka Tanzania bara walishiriki mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku kumi mjini Babati katika mkoa wa Manyara.

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo uwanjani hapo Gekul amewaagiza Wakurugenzi katika halmashauri zote nchini kuwasapoti maafisa michezo na walimu wa michezo ambao wanakwenda vyuoni kusomea kozi ya Michezo katika ngazi mbalimbali.

Aidha amewataka walioshiriki mafunzo hayo wakayatumie katika kuondoa dhulma,upendeleo na kubadilisha mazoea yaliyopo ambayo hupelekea malalamiko katika mchezo huo hapa nchini.

Amewataka viongozi wa CHANETA kuwasilisha katika wizara hiyo changamoto zinazokwamisha maendeleo ya mchezo ili zitafutiwe ufumbuzi.

Gekul amehitimisha mafunzo hayo kwa kusawazisha vyeti kwa washiriki wote 35 waliohitimu mafunzo hayo.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...