Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi amewataka madalali wote nchini wanatakiwa kulipwa na wale wanaowatuma kazi na si vingine.

Wazir Lukuvi azungumza Kauli hiyo Jijini Dodoma leo Novemba 21 wakati akitoa taarifa ya wizara hiyo kwa kipindi cha Miaka 60 tokea Uhuru wa Tanzania Bara.

“Wizara hatuna nia ya kufuta shughuli ya madalali lakini uchukuaji wa vipato vyao umekuwa wa vificho sana na baadhi yao wamekuwa wakifanya vibaya. Inafaa sasa aliyetumwa kazi aliyepwe na aliyemtuma. Tunao ushahidi mar azote wamekuwa wakilipwa kote kote,” amesema Waziri Lukuvi.

Waziri Lukuvi amesema kuwa ameandaa mkutano na madalali nchini ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 13 jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuwapitisha katika muongozo wa wizara hiyo unaosimamia shughuli zao ili serikali ipate kipato kutokana na kazi wanazofanya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...