Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), TANTRADE na TCCIA katika kuimarisha mahusiano wamefanya kikao na menejimenti ya Afreximbank huko Durban - Kwazulu Natal Afrika ya Kusini.

Afreximbank ni bank ambayo inafanya biashara ndani ya Nchi za Africa, inahusika katika Maendeleo ya Viwanda na Mauzo ya Nje, inahusika na biashara za fedha kwa kushirikiana na benk za biashara katika nchi za Afrika na dhamana ya hati fungani. Benk hii ilianzishwa kwa lengo la kufadhili na kukuza biashara ya ndani na nje ya Afrika.

Kikao hicho cha Tanzania na Afreximbank kililenga zaidi katika kuangalia namna bora ambayo benk hiyo itaweza kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Tanzania wanaoweza kushiriki vyema katika soko huria la Afrika kwa kuweza kupata mikopo mbalimbali.
Picha ya pamoja kati ya Timu ya Tanzania na Menejimenti ya Afreximbank. Kutoka kulia ni Bw. George  Mukono Meneja Huduma kwa wawekezaji TIC, Bi. Lizanne Case Kaimu Meneja Ofisi ya Rais Afrieximbank,  Bw. Kudakwashe Matereke Afisa Mtendaji Mkuu wa Afreximbank Afrika Matereke, Bw. Revocatus Radheli Mkurugenzi Huduma kwa wawekezaji TIC, Bi Judith Jeremiah Karangi - Mkurugenzi Mtendaji TCCIA, Bw. Omary Nadr Kaimu Meneja Mahusiano ya wateja Afreximbank na Bw. Fortunatus E. Mhambe Afisa Mkuu wa Biashara TANTRADE.
Pichani ni Mkurugenzi wa  Huduma kwa wawekezaji Bw. Revocatus Rasheli akimkabidhi nyaraka mbalimbali zinazoonyesha fursa za Uwekezaji Bi. Lizanne Case Kaimu Meneja Ofisi ya Rais Afrieximbank.
Bi. Judith Jeremiah Karangi – Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, akimkabidhi Bw. Kudakwashe Matereke Afisa Mtendaji Mkuu wa Afreximbank Afrika Mashariki, Afrika akimkabidhi kablasha lenye fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania baada ya kikao na menejimenti ya Afreximbank Afrika.



Kikao cha pamoja cha timu kutoka Tanzania na menejimenti ya Afreximbank wakijadiliana maswala mbalimbali yanayohusu ya kusaidia uwekezaji, biashara na Intra Africa Trade kati ya nchi ya Tanzania na Afreximbank.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...