MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin
Hasham akizungumza na wananchi mara baada ya kukabidhi matrekta matatu yenye thamani ya milioni 150 |
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham akizungumza na wananchi mara baada ya kukabidhi matrekta matatu yenye thamani ya milioni 150 |
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham kulia akiwa meza kuu kabla ya kukabidhi kukabidhi matrekta matatu yenye thamani ya milioni 150 |
Sehemu ya Matrekta matatu aliyokabidhi Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin
Hasham amekabidhi matrekta matatu yenye thamani ya shilingi Milioni 150
kwaajili ya kuwasaidia wananchi kipindi hiki cha kilimo.
Akizungumza
na wananchi wa kata ya mwanya wakati wa kukabidhi matrekta hayo Amesema
hiyo ni moja ya ahadi yake aliyoiahidi wakati wa kampeni za uchaguzi
wakati akiomba kura hivyo ameona afanye haraka kwani anajua uhitaji wa
matrekta katika jimbo lake ni mkubwa.
Aidha
Mbunge Salim amewatoa hofu wananchi juu ya Taratibu za upatikanaji wa
matrekta hayo kwakuwahakikishia kuwa hayatakuwa na upendeleo wowote bali
kila mwenye uhitaji atakaye toa taarifa katika ofisi yake basi
atapatiwa kwa utaratibu maalum.
Mbunge
Salim Alaudin ameongeza kuwa bado matrekta mengine yanaendelea kuja
hivyo ni vyema wananchi wakayatunza haya matatu ili yatakapo kuja
mengine yaweze kuwasadia wananchi kwa haraka na kuwawezesha kulima
kisasa zaidi.
Wananchi wa
Wilaya ya Ulanga kwa asilimia 80 wanategemea kilimo kwaajili ya
kujiendesha kimaisha hivyo upatikanaji wa trekta hizo utawawezesha
kulima kwa tija nankuwaletea manufaa makubwa bila kuwa na changamoto
kubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...