Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (WUSM) Mhe. Innocent Bashungwa @innocentbash amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya Serikali inayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuijenga Tanzania Mpya.

Mhe. Bashungwa ametoa kauli hiyo leo, Novemba 19, 2021 kwenye kikao kazi na watumishi kikiwa ni kikao cha kwanza tangu Wizara mpya ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuundwa rasmi na kimejadili utekelezaji wa majukumu ya Wizara akiwa na Naibu wake, Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi jijini Dodoma.

Amempongeza Katibu Mkuu wa wizaya hiyo kwa kuwa mbunifu ambapo amesema tayari uongozi wa wizara umekaa pamoja na kujipanga ili kufanya kazi vizuri.

Aidha, amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa fedha takriban bilioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba na kumuagiza Katibu Mkuu kuhakikisha jengo hilo linajengwa kwa ubora unaotakiwa.

Ameyataja baadhi ya mafanikio ya Wizara kwa sasa kuwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mfuko wa Maendeleo ya Michezo, kupunguzwa kodi ya VAT kwa nyasi bandia kwenye viwanja vya Michezo, kurejeshwa kwa Taifa Cup pamoja na kurejeshwa kwa michezo ya (UMITASHUMTA) na (UMISETA).

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Pauline Gekul, amesema kwa sasa nguvu ya Wizara zinaelekezwa katika sekta tatu zilizosalia baada ya kuondolewa kwa Sekta ya Habari ili ziweze kufanya vizuri zaidi.

Awali Katibu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi ametoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli zote hususani kupandishwa madaraja, kulipa malimbikizo ya madai, ununuzi wa vifaa mbalimbali ikiwamo magari ambayo yatawawezesha watumishi zaidi 182 kufanya kazi vizuri.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...