Na. John Mapepele
Wanariadha wa mkoa wa Arusha wamefunika katika mbio ndefu katika mashindano ya Kombe la Taifa (Taifa Cup) yaliyoanza leo katika viwanja vya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Siku ya leo wametawala mbio hizo ambapo kwa upande wa wanawake Mayselina Issa ameshika na nafasi ya kwanza kwa mita 5000,akifuatiwa mshindi wa pili Asha Salim na mshindi wa tatu akiwa Sesilia Ginoka wote kutoka Arusha.
Huku kwa upande wa wanaume mita 10,000 mshindi wa kwanza ni Kaposhi Laizaki kutoka Kilimanjaro, mshindi wa pili Inyasi Sule kutoka Arusha na Joseph Panga kutoka Arusha.
Katika mbio nyingine za mita 800 wanawake mshindi wa kwanza ni Aisha Lubuna kutoka Dodoma, wa pili Mariam Salim kutoka Arusha, na watatu ni Rosemary Justaph kutoka Dodoma.
Huku kwa upande wa mpira wa miguu kwa wanawake Dar imeinga hatua ya fainali ya kwa kitembezea kichapo cha bao 1dhidi ya Dodoma lililofungwa na Nasra Juma katika dakika za 40.
Huku kwa upande wa wanaume Unguja Magharibi imeibuka na kidedea kwa kuichapa Ruvuma bao 1 kwa ambalo limefungwa Mohamed Vuai dakika ya 22 ya mchezo
Kwa upande wa Netiboli wa mkoa wa Dar umeubamiza magoli 46 -30 Dodoma ikiwa na 30 hivyo Dar imetinga fainali, Mjini magharibi imeshinda kwa magoli 56-32 dhidi ya Pwani.
Michezo mingine ya riadha iliyomalizika ni kurusha Tufe ambapo kwa upande wa wanawake Prisila Juma kutoka kusini Unguja kutoka Kusini Unguja amekuwa mshindi wa kwanza akifuatiwa na Tama Jaha kutoka Kusini Unguja na mshindi wa tatu ni Fatuma Khamis kutoka kusini Pemba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...