Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa itakutana Desemba 18, 2021 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu, Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho kitatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuanzia Desemba 15, 2021.
Vikao vyote ni vya kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 toleo la Mwaka 2020 ibara ya 108 (2). Ambavyo vitafanyika Makao Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma ambapo maandalizi ya vikao hivyo yamekamilika.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
SHAKA HAMDU SHAKA
KATIBU WA HALMASHAURI KUU
YA CCM TAIFA ITIKADI NA UENEZI.
14 DESEMBA, 2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...