Waziri Ofisi ya waziri Mkuu - Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe akiongea na wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Misri Hotel ya Hyatt Regency leo tarehe 5 Desemba, 2021 jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya ELSEWEDY Eng. Ahmed Elsewedy akiongea na wafanyabiashara, wawekezaji waliofika kwenye mkutano kati ya Tanzania na Misri Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Steven L. Byabato akiongea na wawekezaji/wafanyabiashara kutoka Misri na Tanzania kwenye mkutano uliofanyika Hyatt Regency leo 05 Desemba, 2021 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda (Zanzibar) Mhe. Omar Said Shaaban akiongea na wafanyabiashara na wawekezaji waliofika kwenye mkutano uliofanyika Hyatt Regency tarehe 5 Desemba, 2021.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Steven L. Byabato akiongea na wawekezaji/wafanyabiashara kutoka Misri na Tanzania kwenye mkutano uliofanyika Hyatt Regency leo 05 Desemba, 2021 Jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara, wawekezaji na viongozi mbalimbali waliofika katika mkutano uliofanyika Hotel ya Hyatt Regency leo 05 Desemba, 2021 jijini Dar esalaam.

MKUTANO wa wafanyabiashara na wawekezaji kati ya Tanzania na Misri umefanyika hotel ya Hyatt Regency leo tarehe 05 Desemba, 2021 jijini Dar es Salaam.

Mkutano huu ulikuwa na lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Misri, kupata taarifa za fursa za uwekezaji zilizopo nchini na vivutio vya uwekezaji. Lakini pia kukutana na taasisi za Serikali zenye miradi ya kipaumbele ambayo inatafuta wawekezaji.

Mkutano huo umehudhuliwa na Waziri Ofisi ya waziri Mkuu - Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe, Waziri wa Biashara (Zanzibar) Mhe. Omar Said Shaaban, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Steven L. Byabato na Mhe. Mohamed Abdel Wahab Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Misri (GAFI) .

Aidha, kufuatia ugeni huu Kituo cha Uwekezaki (TIC) na Mamlaka ya Uwekezaji (GAFI) wamekubaliana kuanza mara moja utekelezaji Mkataba wa Mashirikiano.

Ujumbe huo kutoka Misri una wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya 100 ambao pia watashiriki katika uzinduzi wa mradi wa kuzalisha vifaa vya umeme (Electrical Products) wa kampuni ya ELSEWEDY ElECTRIC EAST AFRICA LTD uliopo maeneo ya Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni kesho 6 Desemba, 2021. Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...