JAJI, Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman amefungua mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa kumi na tano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Mafunzo haya ya siku tano yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yanafanyika kuanzia tarehe 17 Januari mpaka 21 Januari 2022 Chuoni hapo.

Akifungua mafunzo hayo Mhe. Othman aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa mafunzo hayo ni fursa kwao kwani watabadilishana uzoefu kwa kuwa mafunzo hayo yamejumuisha washiriki enye taaluma mbalimbali na sio wanasheria peke yake. Aliendelea kwa kusema kwamba kwa hapa nchini usuluhishi katika migogoro mingi haifanywi na wanasheria bali na wanataaluma wengine.

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Paul. Kihwelo ameeleza lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo maafisa hao wa namna ya kusuluhisha migogoro mbalimbali kati ya watoa huduma na wateja. Mkuu wa Chuo aliongeza kwamba mafunzo haya yatasaidia kuongeza ufanisi katika eneo hilo la usuluhishi wa migogoro.

“Tunaamini mafunzo yatasaidia sana kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi wa kila siku”. Alisema Mhe. Dkt. Kihwelo.

Aidha, Mhe. Dkt. Kihwelo alieleza kuwa Chuo kina jukumu la kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya sheria ili kuwa na uwezo wa kusuluhisha migogoro mbalimbali inayotokea kwenye Mamlaka au Taasisi mbalimbali na kwa kufanya hivyo itapunguza mlundikano wa mashauri mahakamani.

Wakati huohuo Mjumbe wa Bodi na mshiriki wa mafunzo hayo, Bw. Fadhili Manongi ameelezea kwamba mafunzo haya yatawasaidia sana katika utoaji wa maamuzi na kuweza kutenda haki pamoja na kutoa ushauri wa nini kifanyike kuhusiana na migogoro watakayokutana nayo.

Bw. Fadhili ametoa ushauri kwa Mamlaka zote zinazofanya uthibiti, kuja Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kupata mafunzo kama haya.

Mafunzo hayo yamejumuisha maafisa wa EWURA wa ngazi mbalimbali ambao ni Wajumbe wa Bodi na wajumbe wa menejimenti. Mada mbalimbali zitawasilishwa na wawezeshaji mahiri na wabobezi katika masuala ya mbinu za usuluhisi wa migogoro ambao ni Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Faustin Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Robert V. Makaramba Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mhe. Rose Teemba Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
 Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)

Mhe. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akiwa anawakaribisha washiriki wa mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hawapo pichani
Washiriki wa mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
Washiriki wa mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...