Janeth Raphael Michuzi TV

Wizara ya Elimu  Sayansi na Teknolijia imeandaa wiki ya Kitaifa ya ubunifu na
 mashindano ya Kitaifa ya sayansi, teknolojia na ubunifu maarufu kama MAKISATU kwa mwaka 2022.

Wiki ya ubunifu ni Sehemu ya mikakati ya Serikali ya awamu ya sita ya kuongeza hamasa ya matumizi ya sayansi, Teknolijia na ubunifu katika nyenzo nae na kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii

Hayo yamezungumzwa leo February 16, 2022 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolijia Profesa Adolf Mkenda katika kikao chake na waandishi wa habari.

Mkenda ameeleza kuwa Wizara imetenga shilingi  bilioni moja kwa ajili ya kuendeleza watakaoibuliwa katika MAKISATU 2022.,

Wiki ya ubunifu inatarajiwa kufanyika katika Mikoa kumi na Saba (17) Tanzania bara na kwa upande wa Zanzibar pia yatafanyika
Kitaifa wiki ya ubunifu 2022 itawdhimishwa tarehe 15 hadi may, 2022 jijini Dodoma.

"Wiki ya MAKISATU inalenga pamoja na mambo mengine ni kuibua, kutambua na kuendeleza jitihada za wabunifu wa Kitanzania na kuhamasisha matumizi ya Sayansi, Teknolijia na ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii" - Amesema Profesa Mkenda.

 Katika kilele hicho tutakuwa na utoaji tuzo kwa wabunifu 21 walioshinda MAKISATU. Waziri huyo amesema kuwa Usajili wa ubunifu kwa ajili ya Mashindano ulifikia mwisho tarehe 10, Februari, 2022. Lakini kutoka na uhitaji, ametangaza kuongeza muda wa usajili wa Wabunifu hadi tarehe 28 Februari, 2022. Na kusema kuwa Hadi kufikia tarehe 15 Februari, 2022 wamesajiliwa wabunifu zaidi ya 480 kwa ajili ya Mashindano.

Maashimisho hayo yatahusisha pia majukwaa na majadiliano kuhusu maendeleo ya sayansi, Teknolijia na ubunifu nchini.Mafunzo na semina kwa wabunifu ikiwepo elimu ya ujasiriamali na mijadala hiyo itahusisha wabunifu, wadau mbalimbali na Serikali kwa ujumla.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 16,2022  kuhusu maadhimisho ya Wiki  ya Ubunifu na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu maarufu kama (MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambapo kilele cha Mashindano hayo kufanyika Mei 15 hadi 20,2022 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga,akifafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Wiki  ya Ubunifu na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu maarufu kama (MAKISATU) kwa mwaka 2022 kilele cha Mashindano hayo kufanyika Mei 15 hadi 20,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akizungumzia mikakati ya wizara katika kuhusu maadhimisho ya Wiki  ya Ubunifu na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu maarufu kama (MAKISATU) kwa mwaka 2022 kilele cha Mashindano hayo kufanyika Mei 15 hadi 20,2022 jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...