Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mahakama ya hakimu mkazi Njombe imetaja shauri namba 5 la mwaka 2022 linalowakabili Daniel Mwilango na Nikson Nyamideko wanaotuhumiwa na mauaji ya aliyekuwa katibu wa halmashaurui ya welei kanisa la Romani katoliki Kigango cha Parokia ya Makambako.
Akitaja shauri hilo namba 5 la mwaka 2022 hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Njombe Matilda Kayombo amesema watuhumiwa Daniel Mwilango ambae ni katekista mika 42 kabila mbena akishirikiana na Nikson Nyamwideko miaka 23 kabila mbena wote wakiwa wakazi wa Njombe wanadaiwa kuhusika na mauaji ya Nikson Myamba siku ya tar.7 mwezi February mwaka huu.
Wakili wa serikali Magdalena Kisoka akisaidiwa na Paul Ngonyani amesema kosa wanalokabiliwa nalo ni Kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha kanuni ya adhabu Sura ya 16 ya sheria ya mkosa ya jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Hata hivyo hakimu Magdalena Kisoka amepanga tarehe 28 mwezi February kwaajili ya kutajwa tena shauri hilo kutokana na upelelezi wa shauri hilo.
Watuhumiwa wamerejeshwa Rumande kutokana na kesi inayowakabili kutokuwa na dhamana. Ikumbukwe Nikson Nyamwideko na Daniel Mwilango wanashikiliwa kwa tuhuma za kuua na kasha kumkata kata vipande Nickson Myamba siku ya tarehe saba mwezi February mwaka huu katika mtaa wa Mangula Mjini Makambako.
Watuhumiwa wa mauaji wakiingia mahakamani kwa ajili ya kusomewa shtaka lao.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Hakimu mkazi Njombe lililopo Lunyanywi halmashauri ya mji wa Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...