Na Farida Said
VYOMBO vya habari na wanahabari kwa ujumla wameshauriwa kuwa mstari wa mbele katika kupinga sheria kandamizi zinazominya uhuru wa habari na upatikanaji wa habari hapa nchini Ili kutoa uwanda mpana katika uandikaji,uchapishaji na utangazi wa habari kwa lengo la kutoa fursa kwa wananchi kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Mradi wa Boresha Habari Wakili Msomi Godliver Shayo kwenye mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu uandikaji wa habari pamoja na makala katika uwanda wa kilai.
Wakili Godliver amesema kutokana na matukio ya hivi jaribuni ya kufungwa na kufunguliwa kwa vyombo vya habari na kukamatwa kwa baadhi ya waandishi ni moja ya sababu Kituo Cha Sheria na haki za Binaadamu kupitia Mradi wa Boresha Habari kimeona haja ya kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini.
" Kuna tukio la kufunguliwa kwa magazeti ambapo Waziri Nape aliyafungulia magazeti yakiwemo ya Mwanahalisi,Tanzania Daima na Mseto lakini ni vyombo vichache sana ndio vimeripoti kufunguliwa kwa magazeti yale tena na vyenyewe vimeandika kwa juu juu tu, ndio maana tumeona kuna haja ya kutoa mafunzo haya,"amesema Wakili Godliver.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania(TEF) Deodatus Balile amewataka waandishi wa habari nchini kuhakikisha wanafuata Sheria,kanuni na misingi ya uandishi wa habari sambamba na kuwa makini wakati wa utekelezaji wa majukumu hayo.
Kwa upende wao waandishi waliopatiwa mafunzo hayo wamekishukuru kituo Cha msaada wa Sheria na haki za Binaadamu (LHRC)kwa kutoa mafunzo hayo kwani yatawasaidia katika kuandaa mkala za uanda wa kilai zenye ubora na kufuta Sheria pamoja na sera ya habari ya Tanzania.
Mfunzo hayo ya siku mbili yamewakutanisha waandishi kutoka mikoa tofauti nchini ikiwemo Morogoro,Njombe, Mbeya, Dodoma, Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Kiwla, Katavi, Mara, na Arusha ambapo kwa pamoja wamepatiwa mafunzo kuhusu uandishi bora wa makala katika uanda wa kilai pamoja na habari za uchunguzi.
Pia waandishi hao wamepatia elimu kuhusu Sera ya habari nchini sambamba na kanuni pamoja na Sheria ya habari nchini Tanzania.
Home
HABARI
WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA WASHAURIWA KUPINGA SHERIA KANDAMIZI ZINAZOMINYA UPATIKANAJI WA HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...