Na Pamela Mollel,Arusha
Waziri wa Maji Jumaa Awesso,amemteua na kumtambulisha rasmi aliyekuwa akikaimu ukurugenzi wa bodi ya maji bonde lakati,Danford Samsoni,kuwa mkurugenzi wa bodi hiyo ya maji bonde la kati na kueleza Kwamba ameridhishwa na utendaji wake.
Alifanya uteuzi huo jana baada ya kutembelea tanki la kuhifadhi maji, birika la kunyweshea mifugo,vyanzo vya maji ya chemchem katika kijiji cha Qang'dend katika kata ya Mang'ola tarafa ya Eyasi
Alisema tangu kustaafu kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa bodi hiyo,William Mabula na nafasi hiyo kukaimishwa Danford,hajateua wa kuchukua nafasi hiyo kwa sababu alikuwa akiangalia ni nani anae faa hivyo ameridhishwa na utendaji wake na anamtangaza rasmi kuwa mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la kati.
Akitoa salamu zake mbunge wa jimbo la Karatu Daniel Awak,amesema kuwa bila bonde hilo la Mang'ola ,ambalo linalimwa Vitunguu halmashauri ya wilaya hiyo isingelipata maendeleo kwa kuwa asilimia 80% ya mapato ya halmashauri yanatokana na kilimo hicho cha Vitunguu.
Mbunge viti maalumu mkoa wa Arusha kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA , Cecilia Paresso,amepongeza wizara kwa kazi nzuri ya kutekeleza mradi huo wa kuhifadhi chanzo hicho cha maji na kusisitiza kwamba swala la uhitaji maji Karatu bado lipo na ni la muda mrefu.
Katibu wa bonde dogo la Eyasi ,Michael Slaa,amesema kuwa bonde hilo linawanufaisha wananchi ,38120,kutoka vijiji saba,ambapo kumeanzishwa jumuiavza watumiaji maji ambazon pia zina jukumu la kulinda ,kusimami na kutunza vyanzo vya maji,hivyo wanaomba wachimbiwe visima virefu ,marambo ili wakati wa kiangazi wasitaabike kutokana na upungufu wa maji unaokuwepo,pia wameomba wapatiwe ofisi.
Waziri wa maji Jumaa Awesso akikagua eneo la mifugo kunywea maji anayefatia mwenyewe kaunda suti ya blue ni mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la kati Danford SamsonWaziri wa maji Jumaa Awesso akizungumza wakati akimteua Danford Samson kuwa mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la katiKulia ni mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la kati Danford Samson akitoa maelezo kwa Waziri wa maji Jumaa Awesso jana katika ziara yake ya kikazi Wilayani Karatu,Katikati ni Mbunge wa jimbo hilo Daniel Awak kushoto mkuu wa wilaya ya karatu Dadi Kolimba
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...