Na.Khadija Seif, Michuzi TV

WANAWAKE watakiwa kusaidia jamii hususani watoto wenye Mazingira magumu kupitia vipawa vyao Ili kuwapa tabasamu na thamani kama watoto wengine.

Akizungumza na Michuzi, Mbunifu wa Mavazi nchini Ruth Urio maarufu kama Mama j'dore amesema Wanawake Wana nguvu kubwa kuibadilisha jamii kutokana na kuwa walezi bora kuanzia nyumbani Hadi katika ofisi hivyo ni vyema kuwepo utaratibu wa kila Mwanamke mwenye kipato kuikumbuka jamii na kuona Kwa jinsi gani anachangia kuwapa tabasamu watoto.

"Watoto hasa vijijini wanasoma katika Mazingira magumu kiasi kwamba inamkosesha furaha anapoona wenzake wamevaa Mavazi mazuri hivyo Wanawake tukishirikiana Kwa pamoja tunaweza kusaidia watoto wengi sana na kuwapa furaha."

 Mama J'dore amesema kupitia Tamasha lake la Msimu wa 2 wa Mavazi ya ubunifu ya wamama hasa Mavazi ya kistaarab linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Palm village Marchi 29 mwaka huu anategemea zaidi waalikwa kununua nguo ikiwa ni sehemu ya kuchangisha pesa Kwa ajili ya kununua Majora ya vitambaa Ili waweze kuwashona nguo za shule Kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Pamoja na hilo Mama huyo amesema kuelekea Siku ya Wanawake Dunia anaamini Msemo wa Wanawake kushirikiana pamoja kunaleta Mafanikio kutokana na wateja wake Wengi ni wanawake hivyo Kwa kiasi kikubwa anawashukuru Wanawake ambao kadri siku zinavoenda wamekua wakimpa ushirikiano mkubwa

Mbunifu wa Mavazi ya kistaarab Kwa wanawake nje na ndani ya Nchi Ruth Urio maarufu kama Mama j'dore
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...