Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe.Nassor Ahmed Mazrui amesema madaktari bingwa kutoka India wanatarajia kuweka kambi Zanzibar kwa lengo la kuimarisha sekta ya afya nchini.

Akiyasema hayo huko Ofisini kwake Mnazi Mmoja wakati wa hafla fupi ya ujumbe kutoka India uliyofuatana na Mkuu wa Biashara za Kimataifa Somnath Shetty kutoka wockhardt Hospitals LTD .

Alisema ujumbe huo unatarajia kushirikiana na Wizara ya Afya kwa kuimarisha huduma za afya kwa jamii pamoja na utoaji huduma za kesi za upasuaji kwa wagonjwa mbali mbali .

Aidha alisema kesi mbali mbali wanatarajia kuzishughulikia zikiwemo kesi za wagonjwa wanaohitaji kusafirishwa nje ya nchi.

Alifahamisha wajumbe hao wanatarajia kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia sekta ya afya kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu bora kwa wananchi wake .

Waziri huyo alifurahishwa na ujumbe huo wenye lengo la kuisaidia Zanzibar katika utoaji wa huduma za afya na kueleza fursa hiyo itasaidia kuwajengea uwezo pamoja na ujuzi wa kiutendaji kupitia kwa Madaktari Bingwa kutoka India katika hospitali za Mkoa na Wilaya

“Serikali imejenga hospitali nyingi za Wilaya na Mikoa hivyo ni fursa pekee ya kupata wataalamu hao ambao watasaidia kutoa ujuzi kwa wafanyakazi pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi,”alisema Waziri .

Nae Mkuu wa Biashara Kimataifa Somnath Shetty kutoka wockhardt Hospitals LTD amesema lengo la ujio wake ni kuleta mashirikiano ya pamoja katika kuwapatia huduma bora wananchi wa Zanzibar .

Amesema azma yao hiyo ni kuweka kambi ya Madaktari bingwa hapa Zanzibar kwa kutoa huruma mbali mbali za kiafya ikiwemo za upasuaji wagonjwa wenye kesi ambazo zinahitaji kusafirishwa nje ya nchi .

Akitoa Rai kwa wananchi wa Zanzibar aliwataka kukata bima ya afya ya kimataifa ili kuwasaidia kupatiwa huduma ya afya ya nje ya nchi .

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui afanya mazungumzo   na ujumbe kutoka Hospital ya Wockhardt ya Nchini India yenye lengo   la kuimarisha sekta ya Afya Zanzibar ,huko Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi  zawadi maalum mjumbe kutoka Hospital ya Wockhardt ya Nchini India Somnath Shetty,alipofika Ofisini  kwake kujitambulisha.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii , Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui  akipokea zawadi maalum kutoka kwa mjumbe wa Hospital ya Wockhardt  ya Nchini India Somnath Shetty, alipofika Ofisini kwake kujitbulisha 

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...