Mary Margwe, Simanjiro

Agizo la kupeleka Maji Vitongoji vya kijiji cha Langai, wilayani Simanjiro Mkoani Manyara lilitolewa na Makamu wa Rais Dk. Philip Isdori Mpango, limeanza kutekelezwa, ambapo jumla ya wakazi wapatao 4000 watanufaika na mradi huo.

Dk.Mpango alitoa agizo wakati alipokua akiwahutubia wanchi wa wilaya hiyo alipokwenda kuweka jiwe na Msingi mradi mkubwa wa Maji Ruvu Orkesumet, wilayani humo mnano March 15, 2022, ambapo pamoja na mambo mengine alizindua wiki ya Maji Kitaifa Wilayani Simanjiro.

Aidha kufuatia kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo, Diwani wa Kata ya Langai Mh.Jackson Sipitieck ameishukuru serikali kwa kuanza utekelezaji wa mradi huo, mbapo anafafanua kuwa kwa sasa wananchi wanaendelea kununua ndoo moja ya Maji kwa sh.500, hivyo ujio wa mradi huo utawasaidia kuwanufaisha zaidi ya wakazi wapatao 4000, hivyo mradi huo utakua no mkombozi mkubwa kwa wananchi wa vitongoji vya Kijiji cha Langai.

" Tunaishukuru sana serikali yetu ya awamu ya sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanza kutekeleza agizo ama ahadi ya Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, kama mnakumbuka siku ile ya zira yake wilayani kwetu mnamo Mach 15 , mwaka huu alisema maji ni lazima yafike kijiji cha Langai, na kweli kama mnavyomuona Mhandisi wa Maji hapa amekuja na wataalam kutuonyesha vituo 8 na pia kitakua na matanki makubwa mawili ya kusambaza maji, hivyo ahadi ya Mh.Dk.Mpango imeanza kutekelezwa" alisema Sipitieck.

Aidha Sipitieck alisema serikali ya chama cha mapinduzi iko kazini na kazi inaendelea usiku na mchana, hivyo wananchi wana kila sababu ya kuendelea kuiamini serikali ya Ccm chini ya Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Samia Suluhu Hassan.

Sipitieck pia aliwatahadhalisha wananchi kuhusiana na kuondoa kabisa mawazo ya kulipwa fidia maeneo yatakayo pita mabomba ya Maji, kwani hayo Maji ni kwa faida ya wananchi wote, hivyo maeneo hayo yatakayochimbiwa mabomba watakua wamejitolea ili kuweza kufanikisha kupata huduma hiyo ya maji.

" Mradi tumeupokea na tunaahidi kuulinda kwa namna yoyote ile, kwa gharama yoyote na kuuwezesha kuwa endelevu ili kuhakikisha unatusaidia sisi na vizazi vyetu vijavyo, lakini mmeambiwa hapa na Mhandisi Mush kuwa hakutakuwa na fidia kwa mtu yeyote atakayepitiwa na mradi huu, hivyo ni lazima kila mmoja wetu aondoe mawazo ama fikra ya kufikiria kwamba kutakua nakulipwa fidia, huu ni mradi wetu hivyo utakuja kutunufaisha sisi wenyewe" aliongeza Mh.Sipitieck.

Aidha Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mhandisi Danie Mush alisema mradi huo utakuwa na vituo 8 vya kuchotea maji, matanki makubwa mawili, pia kutakua na mtandao mkubwa wa bomba utajaokua na km. 21.

Mhandisi Mush alisema lengo ziara yao ni kwenda kuutambulisha mradi kwa wananchi ili waujue pamoja kukubaliana juu ya kutokulwepo kwa fidia kwa wananchi wowote wale watakaopitiwa na mradi huo ili walifahamu hilo mapema.

" Nimewaletea habari njema, kimsingi katika mwaka huu wa fedha, tumekuja kuutambulisha mradi huu wa maji ambao utakua na vituo vinane vya kuchotea maji, matanki makubwa mawili, pia kutakua na mtandao mkubwa wa bomba utajaokua na km. 21, tunachotaka kwenu ni kutoa ushirikiano ,tutakuja kukaa nanyi ili tuunde kamati itakayoahili watu ili kidogo kitakachopatikana kwenye ulipaji wa maji tuwawalipa wale wasimamizi wa maji, si hatuwezi jamani watu wafanye kazi alafu tusiwalipe kaposho, ili kuwezesha ule mradi uwe endelevu, alisema Mhandisi Mush

Hata hivyo mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Langai Helena Laizer alisema kwa sasa maji wananunua ndoo moja kwa sh. 500, hivyo ujio wa mradi huo kwao utakua ni mkombozi mkubwa katika maisha yao, hivyo ameahidi kuulinda huo mradi ili kuwezesha kuwa endelevu na hatimaye kuweza kuwasaidia vizazi hata vizazi.

Diwani wa Kata ya Langai wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Jackson Sipitieck, akizungumza na wananchi wa vitongoji vya Kijiji cha Langai kuhusiana na utambulisho wa mradi wa Maji ambao ilikuwa ni ahadi ya Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango wakati alipokua na ziara wilayani Simanjiro Machi 15, 2022 kwenye uwekaji wa jiwe la msingi mradi mkubwa wa maji Ruvu Orkesumet, ambapo jumla ya wakazi wapatao 4000  watanufaika na mradi huo ambao ahadi hiyo imeanza kutekelezwa, Picha na Mary Margwe






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...