NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO.
Mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Shafii Saidi Mwinyingoma alisema wazee wa wilaya ya Namtumbo wamempatia jina la Mndendeule nambari moja mkuu wa wilaya ya Namtumbo kwa namna anavyoshirikiana bega kwa bega na wananchi wa wilaya ya Namtumbo.
Mwinyingoma alisema hayo akiwa ikulu ndogo wilayani Namtumbo ambapo mkuu wa wilaya ya Namtumbo aliandaa chakula cha jioni kwa ajili ya futari kilichoandaliwa kwa ajili ya wazee wa wilaya ya Namtumbo.
Hata hivyo Mzee Mwinyingoma alimtaka mkuu wa wilaya huyo kudumisha ndoa yake kwa kuwa mafanikio yake ya uongozi katika wilaya ya Namtumbo yanatokana pia na ushauri wa ndoa yake kuwa imara na kumfanya afanye kazi zake vizuri.
Shafii Mwenyeheri Shekh wa wilaya ya Namtumbo pamoja na kumshukuru mkuu wa wilaya huyo kwa kuwaheshimu na kuwajali kwa kuwaandalia futari alisema ni dalili za kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati ya wazee wa Namtumbo pamoja na ofisi yake.
Mwinyiheri alisema wazee wa wilaya ya Namtumbo na waislamu wa wilaya ya Namtumbo wanamhakikishia ushirikiano wa dhati kwa ajili ya kuiendeleza Namtumbo kupitia uongozi wa mkuu wa wilaya Huyo.
Faraji Amiri Kifunga mwenyekiti wa bakwata wilaya ya Namtumbo pamoja na mambo mengine alimshukuru mkuu wa wilaya kwa kuwajali wazee na waislamu wa wilaya ya Namtumbo na kukiita kitendo hicho ni kitendo cha kuimarisha mahusiano ,upendo na ushirikiano kati ya ofisi yake na wananchi wa wilaya ya Namtumbo.
Nuru Isumairi Matambo akiongea kwa niaba ya akina mama waliohudhuria chakula cha jioni kwa ajili ya futari alisema anamshukuru mkuu wa wilaya huyo kwa jitihada yake ya kuwakutanisha akina mama katika chakula cha jioni na kuwafanya waweze kufahamiana ,kutambuana hasa kumtambua mke wa mkuu wa wilaya huyo na kushirikiana naye katika chakula cha jioni na mambo mengine yajayo kwa kuwa amewajengea mahusiano kupitia chakula hicho cha jioni alisema Nuru.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu aliwashukuru wazee wa Namtumbo kwanza kwa kujitokeza kuja kuitika wito wake wa kuwaomba wazee hao kushiriki chakula cha jioni naye ikulu ndogo mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo.
Dkt Ningu alisema kitendo cha kujitokeza kuja alidai wazee hao wamemheshimisha kwa kiasi kikubwa kwani kuandaa chakula cha jioni ni kitu kingine na wananchi kujitokeza kuitika wito ni kitendo cha kuniheshimisha alisema mkuu wa wilaya huyo.
Aidha Dkt Ningu pamoja na kuwashukuru wazee wa wilaya ya Namtumbo aliwathibitishia wazee wa Namtumbo kwa kuwapa ushirikiano katika ofisi yake kwa lengo la kuipeleka Mbele kimaendeleo wilaya ya Namtumbo.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu amepewa Jina la Mndendeule nambari moja wilaya ya Namtumbo kwa kile kinachodaiwa kabila kubwa wilayani Namtumbo ni wandendeule na yeye ndiye nambari moja likifuatia kabila la wayao,wanindi ,wamakua na wangoni kwa kiasi kidogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...