Na Amiri Kilagalila,Njombe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini kuwaelimisha na kuwahamasisha wafuasi na wanachama wa vyama vyao ili waweze kuhesabiwa katika zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika mwezi wa nane mwaka huu.
Mpango ametoa wito huo mkoani Njombe wakati akizindua mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa katika uwanja wa Saba saba mjini Njombe.
“Ninawaomba viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wetu wa dini na viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kelimisha na kuhamasisha wafuasi au wanachama wao kuhesabiwa tarehe 14 mwezi wa 8 mwaka huu wa 2022”alisema Mpango
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...