Na Mwandishi Wetu, TANGA
Kikao Kazi na Mafunzo kwa Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya nchini kimeanza leo tarehe 4 April 2022 mkoani Tanga.
Kikao hicho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete.
Katika kikao hicho pamoja na uwasilishwaji mada, Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya nchini watapata mafunzo ya namna bora ya kuendesha mashauri ya ardhi pamoja na uandishi mzuri wa hukumu.
Katika siku ya kwanza ya kikao hicho Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi Benhaji Masoud aliwasilisha mada kuhusiana na masuala mtambuka katika uendeshaji mashauri ya ardhi.
Kikao hicho cha siku nne kinatarajiwa kumalizika siku ya alhamisi tarehe 7 April 2022.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Michael Luena akizungumza katika kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4
April 2022
Sehemu
ya Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wakiwa katika
kikao kazi na mafunzo cha wenyeviti hao kinachoendelea mkoani Tanga
tarehe 4 April 2022.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi Benhaji Masoud
akiwasilisha mada kwenye kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza
ya Ardhi na Nyumba kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022.
Msajili
wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stella Tullo akizungumza wakati
wa kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya
Wilaya kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Zakariyya Kerra akizungumza katika kikao Kazi na Mafunzo cha
Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kinachoendelea mkoani
Tanga tarehe 4 April 2022.
Sehemu
ya Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wakiwa kwenye
kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti hao kinachoendelea mkoani Tanga
tarehe 4 April 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...