Na Fredy Mshiu

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) ni miongoni mwa wadau wa sekta ya maji walioshiriki kongamano la Kisayansi la Maji linalowakutanisha Taasisi na Mashirika mbalimbali linalofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es salaam.

Akifungua kongamano hilo, Naibu Waziri wa maji Mhe.Maryprisca Mahundi (Mb) amesema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wadau wa sekta ya maji kujadili kwa pamoja tafiti mbalimbali zilizofanyika na zitakazoleta matokeo chanya katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji.

"Kongamano hili ni muhimu sana katika kuandaa sera zetu za uendelezaji wa rasilimali maji lakini pia kuangalia uwezekano wa kutumia ili kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za usimamizi wa rasilimali hizi" aliongeza Mhe Mahundi

Mkuu wa chuo cha Maji, Dkt Adam Karia ambao ni waandaaji wa kongamano hili alisema lengo la kuandaa kongamano hili ni kujadili na kuiboresha sekta ya maji kupitia wataalamu mbalimbali walionao na wanaoendelea kuingia katika sekta ya maji.

"Naishukuru Serikali kwa kuendelea kuthamini juhudi mbalimbali zinazotekelezwa na Chuo Cha Maji hususani katika kuandaa kongamano hili litakalowakutanisha wadau zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali ili kuendelea kuhakikisha changamoto katika sekta ya maji zinapatiwa ufumbuzi " alisema Dkt Karia

Kwa upande wa DAWASA, Meneja Mawasiliano Bi Everlasting Lyaro amesema ushiriki wao kama Mamlaka ni kupata nafasi ya kujifunza na kupitia kwa kina tafiti zilizopitiwa ambazo zinaweza kutoa ufumbuzi wa changamoto katika sekta ya Majisafi na Usafi wa Mazingira.

"Sisi kama Mamlaka tunatumia nafasi hii kukutana na kusikiliza tafiti mbalimbali za wadau wa sekta ya Maji ili kuweza kupata ufumbuzi wa mambo mbalimbali yahusuyo huduma za maji. Ni wakati muafaka wa Serikali kuzipa kipaumbele tafiti hizi zilizoandikwa na wabobezi ili zikatoe majibu ya sera mbalimbali za sekta" alisema Lyaro

Naye, Makoye Richard Mtaalamu wa Maabara kutoka Idara ya Rasilimali Maji kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam amesema Chuo kama wadau wa sekta ya maji wamekuwa mstari wa mbele katika kuandaa wataalamu watakaosaidia kutoa majawabu kwa changamoto mbalimbali katika sekta nyingi hapa Nchini.
"Chuo kikuu Dar es salaam ni moja ya vyuo vilivyojikita zaidi katika kusimamia tafiti zenye tija kwa Taifa lakini pia kuangalia namna tafiti hizo zinavyoenda kutumika katika kuleta ustawi wa Jamii hususani katika nyanja ya sayansi ambayo ndio mkombozi wa maisha ya Binadamu" alisema Ndugu Makoye

Kongamano la pili la Kisayansi katika sekta ya Maji linafanyikana kauli mbiu "Usimamizi wa Rasilimali za maji kwa huduma endelevu za usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira" linafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 04.04.2022 hadi 05.04.2022 huku taasisi zaidi ya 20 zikishiriki kongamano hilo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...