Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameahidi kushirikiana na watendaji na watumishi wa Wizara yake katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Wizara hiyo.

Ameyasema hayo leo Aprili 2,2022 alipowasili katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zilizopo Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa.

“Niwahakikishie kwamba niko tayari kuchapa kazi pamoja nanyi,  imani kubwa ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametupa hatutamuangusha” Mhe. Chana amesisitiza.

Aidha, ameweka bayana kuwa yuko tayari kufanya kazi kwa saa 24 bila kikwazo chochote. 
"Mimi kama  Waziri  wenu  milango iko wazi saa 24, hakuna wakati sitapatikana iwe ni usiku, iwe asubuhi hata iwe sikukuu na ndio maana ya kuwa mtumishi wa umma.” Amesisitiza.

Naye, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) ameeleza kuwa Wizara imepata mtu sahihi wa kuitoa ilipo na kuisogeza mbele na kwamba Mhe. Pindi Chana yuko na timu ya watendaji mahiri na wachapakazi. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amemkaribisha Waziri Pindi Chana na kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

“Tunakukaribisha sana katika Wizara ya Maliasili na Utalii na kukupongeza sana kwa kuteuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Maliasili na Utalii”amesema Mhe. Masanja 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameanza kazi leo kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...