BENKI ya NBC yaandaa Chakula cha Jioni kwaajili ya wateja wake katika hoteli ya Hyatt Regancy the Kilimanjaro jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwajili ya kujadili matarajio ya siku zijazo.

Katika Chakula hicho cha jioni kuliundwa jukwaa la benki hiyo kwaaajili ya Kubadilishana mawazo na kujadiliana na wateja wake changamoto zinazowakabili.

Hata hivyo waliangalia malengo yajayo benki hiyo baada ya kudorora kwa biashara kwa miaka miwili kutokana na janga la Covid-19.

Mkurugenzi Mkuu wa NBC Tanzania, Theobald Sabi akiongozana na Mtendaji Mkuu wa Uendeshaji wa ABSA Kanda iliwakaribisha watendaji wakuu wa biashara kutoka viwanda 50 nchini kwa lengo la kufungua fursa za biashara katika soko la Afrika.

Wateja wa Benki ya NBC wakisalimiana wakati wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na benki yao jijini Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki.
Wateja wa Beki ya NBC wakiurahia vinywaji wakati benki yao walipoandaa chakula cha jioni kwaajili ya kuzungumza nao juu ya matarajio ya benki hiyo kwa siku zijazo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...