Na. Farida Ramadhan, WFM, Dodoma
Serikali
imeeleza kuwa Sheria ya Kudhibiti Utakasishaji wa Fedha Haramu,
Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi haihusiki na
utoaji dhamana kwa watuhumiwa wa makosa ya kawaida.
Hayo
yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad
Hassan Chande alipojibu swali la Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus
Mwanyika, aliyetaka kujua wakati ambao Serikali itarekebisha Sheria ya
Utakasishaji Fedha aliyodai inazuia dhamana kwa watuhumiwa hata kwa
makosa ya kawaida.
Mhe. Chande alisema hakuna sababu ya
kurekebisha Sheria hiyo kwa kuwa kifungu cha 12 cha Sheria hiyo SURA
423, kinabainisha makosa ya utakasishaji fedha haramu pekee na
hakihusiki na masuala ya dhamana kwa makosa ya kawaida.
“Utaratibu
wa dhamana kwa makosa mbalimbali, ikiwemo utakasishaji wa fedha haramu
unasimamiwa na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, SURA 20”,
alifafanua Mhe. Chande.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...