Na Pamela Mollel,Arusha
Katibu
Mkuu wizara ya maliasili na utalii Dkt Francis Michael amegawa vifaa
vya kujikinga na Uviko 19 ikiwemo barakoa 140,000 na vitakasa mikono
14,285 kwa vyama vya utalii ikiwa ni maandalizi ya kupokea idadi kubwa
ya watalii hapa Nchini
Alifanya zoezi hilo la ugawaji wa vifaa hivyo leo jijini Arusha wakati alipokutana na wadau wa utalii
Alisema
kuwa jitihada mahsusi za Mh Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania za
kutangaza Tanzania kimataifa kupitia programu maalumu ya Royal tour
ambayo imeenda sambamba na kuimarisha mapambano dhidiya ya UVIKO 19
Dkt
Francis alisema kuwa wizara imejipanga kushirikiana na wadau ili
kuendeleza programu ya Royal tour kwa lengo la kuvutia watalii kutoka
masoko mbalimbali kutembea Tanzania na kuongeza mapato
Pia
alisema kuwa kutokana na ushawishi wa Mh.Rais serikali ilipokea fedha
za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko
ambapo sehemu ya fedha hizo zimetumika kuimarisha sekta ya utalii hapa
nchini
"Fedha
hizo zimetumika kukarabati kilometa 2,383.12 za barabara katika maeneo
ya hifadhi za Taifa ikiwemo mapori ya Akiba,Tengefu na misitu ya hifadhi
ya mazingira ya Asili"Aliaema Dkt Francis
Aliongeza
kuwa fedha hizo za uviko zimekarabati viwanja vya ndege katika hifadhi
za Taifa pamoja na kujenga malango 14 ya kupokelea wageni katika maeneo
ya hifadhi sambamba na kuboresha mazingira ya biashara
Kwa
upande wake katibu mtendaji wa shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania
Richard Rugimbana akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo kwa
niaba ya vyama hivyo alisema kuwa ni vyema msaada huo ukatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa
"Hapa
mbele yako Mh Katibu Mkuu tuna vyama 10 na hivi vyama vidogo ndivyo
vinakutana na watalii na mfano mzuri ni namna wanavyowapandisha watalii
mlima Kilimanjaro na maeneo mengine ya utalii"alisema Rugimbana
Alipongeza Serikali katika jitihada za kutangaza utalii sambamba na kuchukua tahadhari za Uviko 19
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...