Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMATI Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) inarajiwa kukutana jijini Dar es salaam kesho chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga pamoja na mambo mengine Kamati itapokea taarifa mbalimbali ya utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa 12 wa Baraza hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa jana na Katibu Mtendaji wa TNBC, Dkt Godwill Wanga, maandalizi ya kikao hicho muhimu yamekamilika ambapo Kamati itapitia taarifa na hatimaye kutoa mwongozo.
“Wajumbe wa Kamati Tendaji inawajumuisha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali kwa upande wa Serikili na upande wa Sekta Binafsi ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi pamoja na wajumbe wote wa Bodi ya Wakurugenzi,” alisema.
Dkt Wanga alisema kikao cha Kamati Tendaji kinatakiwa kufanyika kabla ya Mkutano wa 13 wa Baraza unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo ambao utaongozwa na Rais Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza.
Alisema wajumbe wa Kamati watapitia muhtasari wa Kikao Maalumu cha 42 cha Kamati Tendaji kilichofanyika juni 17, 2021 pamoja na kupitia Rasimu ya Kitabu cha Mkutano wa 13 wa TNBC na kuidhinisha Nyaraka za Kiutawa za TNBC.
“Wajumbe pia watapata nafasi ya kupata taarifa za utekelezaji wa Mpango kazi Blue Print, Nyaraka ya Tathmini ya Mfumo wa Mapato na Matumizi ya Serikali, Tathmini ya Sekta ya Utalii na Regulatory Impact Assessment (RIA),” alisisitiza.
Baraza kama taasisi ni chombo muhimu kwa kuzikutanisha sekta za Umma na Binafsi pamoja na kuweza kufanya mashauriano kwa pamoja kwa manufaa na faida za kijamii na kiuchumi kwa watanzania wote.
Kuanzishwa kwa TNBC takribani miongo miwili iliyopita, mafanikio makubwa yamepatikana ikiwemo kukua kwa sekta binafsi hapa nchini sambamba na kuongezeka kwa kuaminiana kati ya sekta hizo mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...