Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi na
Mawasiliano wa DRC Congo Cherubi Senga na Waziri wa Ujenzi na
Mawasiliano wa Burundi, Marie Nijimbe katika picha ya pamoja na
watendaji mara baada ya kusaini ripoti ya watalam ya Mradi wa Reli ya
Kisasa ya SGR ya Uvinza-Musongati-Gitega-Bujumburaa-Uvinza-Kindu wenye
Jumla ya Kilomita 939, mjini Kinshasa.
Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi (kushoto) akiwa na Makatibu wa Wizara zinazosimamia Uchukuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi wakisaini ripoti ya Wataalam ya Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Uvinza-Musongati-Gitega-Bujumburaa-Uvinza-Kindu wenye jumla ya Kilomita 939, mjini Kinshasa.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (kulia) akiwa na Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wa DRC Congo Cherubi Senga (katikati) na Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wa Burundi, Marie Nijimbe (kushoto) wakionyesha taarifa ya watalam ya Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Uvinza-Musongati-Gitega-Bujumburaa-Uvinza-Kindu wenye Jumla ya Kilomita 939, uliofanyika mjini Kinshasa mara baada ya Mawaziri hao kuisaini mjini Kinshasa.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika mkutano uliwakutanisha Mawaziri wanaosimamia Uchukuzi wa Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Makatibu Wakuu na Wataalam wa nchi hizo (hawapo pichani) kujadili na kusaini ripoti ya Wataalam ya Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Uvinza-Musongati-Gitega-Bujumburaa-Uvinza-Kindu wenye Jumla ya Kilomita 939, mjini Kinshasa.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...