Na. Catherine Sungura,WAF-Dodoma
Serikali
kupitia Wizara ya afya inatarajia kukamilisha mkakati wa utoaji wa
huduma kwa wagonjwa wa afya ya akili ikiwemo afya ya akili
mashuleni,kazini pamoja na kwenye jamii.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Tiba Dkt. Omary ubuguyu wakati
wa mahojiano na Televisheni ya Channel Ten wakati wa kipindi cha
baragumu mapema wiki hii.
Dkt. ubuguyu alisema
mkakati huo unatarajia kutoka mwaka huu ambapo utajikita katika sehemu
tatu ikiwemo afya ya akili mashuleni na kutaja kuwa sehemu kubwa ambayo
watu wanaweza kupata shida na magonjwa mengi ya afya ya matatizo ya
akili yanatokea kabla ya miaka 25.“Aidha, changamoto kubwa zitatokea
hapo chini au wagonjwa wengi wataonekana kwenye umri huo”.
Kwa
sehemu ya afya ya akili makazini Dkt. Ubuguyu alisema sehemu hiyo ndio
inayoathiri kwa kiwango kikubwa kuliko sehemu yoyote na kuongeza kuwa
sio sehemu za ajira rasmi tu bali ni sehemu yeyote ambayo watu wanapata
kipato ikiwemo sokoni na kutolea mfano soko linapounguahivyo mkakati huo
utaenda kuangazia eneo hilo.
Dkt. ubuguyu
ametaja pia sehemu ya tatu ni afya ya akili katika jamii ambap ndio
ombwe kubwa kwani taktika jamii unapotaja afya ya akili watu huanza
kucheka na kuona magonjwa au shida mbele badala ya kuonekana afya kwa
ujumla wake kwani watu wanapowasiliana ni kwamba afya zao za akili zipo
sawa.
Hata hivyo Dkt. Ubuguyu alisema suala la
afya ya akili Wizara ya afya imelipa kipaumbele ikiwemo maboresho ya
miundombinu kwenye hospitali ya Taifa ya afya ya Akili ya Mirembe pamoja
na hospitali za rufaa za mikoa.
“Uwekezaji
katika miundombinu na kwa watoa huduma ambapo hivi sasa tumefanyia
maboresho makubwa kwenye Hospitali ya Taifa ya afya ya akili ya Mirembe
hospitali za rufaa za mikoa 11 kati ya 28 zinatoa huduma za afya ya
akili hasa huduma za kulaza”.Alisema
Kwa
upande kwa kukabiliana na changamoto ya afya ya akili ni utoaji wa
elimu kwa ujumla kwa maana watu waelewe kuhusiana na masuala ya afya
ya akili na si kusubiri kushughulika na watu wenye Magonjwa ya akili.
Aliongeza
kuwa Wizara ya Afya inayo jukumu kubwa la kushughulikia afya ya
akili pamoja na Wizara ya maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalumu ambayo inashughulikia na afya ya akili aidha, inayo
watu wenye makundi maalumu hivyo kuhakikisha watu hao hawapati
changamoto za afya ya akili
Changamoto ya afya
ya akili Kitaifa Dkt. Ubuguyu alisema hali ni mbaya na sio tu Tanzania
bali dunia nzima na kuongeza kuwa sehemu kubwa ya ukatili imebebwa na
sehemu ya malezi kuanzia kwa watoto ambapo makuzi yanakuwa sio mazuri
kwani wazazi wamekubwa ‘busy’ kutafuta maisha na hali ya kuchangamana
na watu ikiwemo mitandao ya kijamii.
“Uchochoe
wa vurugu na matatizo kwenye jamii ni ukorofi pamoja wazazi wengi
huelekeza watoto kwa kupiga hivyo ukatili huo humfanya mtoto kujua hayo
ndio maisha na hivyo inakua rahisi kuwa na ukatili kwa jamii tofauti na
zamani ambapo watoto walikua wakipelekwa kwa babu na bibi zao”.
Dkt.
Ubuguyu alitoa wito wa jamii na familia kwa ujumla kuacha tabia ya
ukatili kwa watoto na hivyo kujenga mazoea ya kukaa na kuongea pamoja
kama familia kwani dunia imebadilika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...