Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

WAKAZI zaidi ya 3,500 wa Mitaa ya Mwanalugali A na B ,kata ya Tumbi ,wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani wanatarajia kuondokana na kero ya kutembea umbali wa kilometa kumi kufuata huduma za afya kituo cha afya Mkoani na hospital ya Rufaa ya Tumbi baada ya ujenzi wa Zahanati ya Mwanalugali kukamilika mwezi septemba mwaka huu.

Ujenzi huo Hadi Sasa umefikia asilimia 70 ambapo umeanza mwezi march mwaka huu.

Akitembelea mradi wa miundombinu ulioibuliwa na wananchi na kufadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) , Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alitoa agizo kwa mganga Mkuu wa mkoa kuhakikisha wanaandaa wataalamu na watendaji wa afya mapema ili mradi ukianza wawepo tayari.

Agizo jingine Ni kuwepo kwa vifaa tiba ili huduma zianze Mara moja baada ya ukamilishaji wa mradi huo.

Pia Kunenge amemuagiza, mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, na wataalamu wake kupima na kuandaa mchoro na Hati kwa eneo hilo ili kuondoa changamoto za migogoro ya ardhi isije kujitokeza baadae .

Pamoja na hayo ,ameitaka Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) na  Shirika la Umeme ( TANESCO) kuweka Mazingira mazuri ya upatikanaji wa huduma hizo wakati wa utoaji huduma Sambamba na TARURA ihakikishe inachonga barabara zote zinazoelekea katika Zahanati ya Mwanalugali ili kuondoa usumbufu.

Awali mkazi wa Mwanalugali, Frida Mvalla ,alieleza mradi huo utakuwa mkombozi kwao kwani walikuwa wakipata shida hasa kwa wajawazito na Watoto pamoja na kuhangaika endapo kunatokea wagonjwa nyakati za usiku.

Nae Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Mji wa Kibaha,Anita Lioka alisema , wananchi wameibua mradi huo na TASAF imefadhili ambapo utagharimu kiasi cha sh.milioni 113.6.

Alitaja changamoto za mradi kuwa ulisimama wiki mbili kutokana na mvua na ,ongezeko la vifaa .

Licha ya hayo ,wanaomba kuongezwa jengo la kujifungulia ili kusaidia wakinamama na watoto .

"Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha jamii kupitia fedha za TASAF na kusaidia kaya maskini,Kwakuwa itasaidia kuwaondolea kero wananchi hawa",

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...