Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
TIMU ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kufuzu raundi nyingine ya kuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN) ambapo itakabiliana na Uganda kwenye mchezo wa mwisho wa mchujo ‘Play Off’.
Taifa Stars itacheza na Uganda (The Cranes) baada ya ushindi wa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya timu ya taifa ya Somalia kwenye michezo miwili iliyochezwa katika dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Kwenye mchezo wa mkondo wa pili, Stars imapata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Somalia, mabao hayo yamefungwa na Abdul Suleiman Sopu dakika ya 34 na bao la pili likifungwa kwa mkwaju wa Penalti na Mlinzi, Dickson Job wakati bao la Somalia limefungwa na Farhan Ahmed dakika ya 47 baada ya ‘reflection’ ya Bakari Mwamnyeto.
Mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Julai 23, 2022 kwenye uwanja huo huo, Stars walishinda bao 1-0, bao pekee la Mshambuliaji Abdul Suleiman Sopu, hivyo kufanya jumla ya mabao 3-1 kwenye michezo yote miwili.
Mshindi wa jumla wa mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda atafuzu Michuano ya CHAN ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Algeria, kuanzia Januari hadi Februari, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...