Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, ameshiriki pamoja na wana CCM wa Kata ya Oysterbay kuwachagua viongozi wapya wa Chama katika kata hiyo.

Uchaguzi huo umefanyika leo Agosti 6, 2022 katika Shule ya Msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wamechaguliwa.

Akiwasalimia wana CCM wenzake baada ya upigaji kura, Kinana amesema Chama kinafurahishwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali na kufanya uchaguzi kwa amani.

Kinana amesema hadi sasa mwenendo wa u haguzi unakwenda vizuri na kwamba changamoto chache zinazojitokeza hususani kuhusu  malalamiko ya ukiukwaji wa haki, hatua zitachukuliwa na haki itatendeka.

"Yapo malalamiko ya hapa na pale, lakini nina hakika yatafanyiwa kazi ili mwanachama akishinda ashinde kwa haki. Msingi wa Chama hiki ni kutenda haki, kwa hiyo nina hakika viongozi watatenda haki," amesema Kinana.

Nafasi zilizopigiwa kura ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Oysterbay, wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa, wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya na wajumbe wa halmashauri kuu ya kata hiyo.








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...