*Msanifu wa Majengo Kondoro kujenga majengo bora ni wajibu wetu

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Wakala Majengo (TBA) wamefanya kazi nzuri katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Amesema ujenzi huo umegharimu sh.Bilioni ni sita ambazo fedha hizo zimefanya kazi nzuri na jengo likiwa bora jengo.

Rais Samia aliweka Jiwe la Msingi katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya hivi karibu Jijini hapa ambapo alisistiza ujenzi uendane na thamani ya fedha (Value for Money).

Rais Samia amesema kuwa alirushiwa picha ya jengo analokwenda kuzindua na kuona jengo limejengwa vizuri na kwa uimara zaidi.

Aidha Rais Samia alisema kuwa wanaendelea kujengo majengo yaliyo bora kwani hata majengo ya mahakama wameanza kuyaboresha kwa kiwango kinachohitajika.

‘’Jengo hili limetumia Sh. Billioni Sita ,Mbeya ndio Makao Makuu ya Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini lazima kuwe na jengo linaloendana na Makao Makuu tutaendelea kujenga majengo ya aina hii,katika kila mikoa iliyokuwa Makao Makuu ya Kanda.

‘’Nimeridhika na sena ilivyotumika ,nawapa pongezi wanambeya, Fedha ilivyotumika, imeendana na uhalisia’’, alisema Rais Samia

Mbeya niwaambie furaha yangu kuona jengo la Mkuu wa Mkoa, jengo hili litahudumia wananchi wengi.

Naye Mtendaji Mkuu wa TBA Msanifu wa Majengo Arch. Daud Kandoro amesema kwanza anamshukuru Rais kwa kuzindua jengo hili, lakini wao ni wajibu wao kujenga majengo ya Serikali tena kwa ubora wa hali ya juu.

Arch. Kandoro amesema utayari wao upo wakati wote wanapohitajika kwani ubunifu huu umeanzia ofisini TBA na ubunifu wa mji wa Serikali Dodoma walifanya TBA na kushiriki kujenga.
Rais Samia Hassan Suluhu akizindua Jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lililojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania(TBA).
Wafanyakazi wa TBA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa  Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya aliyelizindua Rais Samia Hassan hivi karibuni.
Msanifu wa Majengo wa TBA Daud Kondoro mwenye suti ya samawari (Blue) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi mara baada ya kuzindua Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lililozinduliwa na Rais Samia Hassan Suluhu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...