

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani Dar es salaam, Agost 3, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chombo kinachoonyesha ramani ya kiwanda cha kuchakata gesi asilia kinachotarajiwa kujengwa mkoani Lindi wakati alipotembelea banda la makampuni ya Shell na Equinor baada ya kufungua Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani Dar es salaam, Agost 3, 2022. Kulia ni Makamu wa Rais na Meneja wa Kampuni ya Uquinor nchini, Unni Merethe Fjaer na katikati ni Makamu wa Rais na Mwenyekiti wa Kampuni ya Shell nchini, Jared Kuehi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati, January Makamba katika Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania alilolifungua kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani Dar es salaam, Agost 3, 2022
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua kongamano hilo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani Dar es salaam, Agost 3, 2022.
Waziri wa Nishati, Januari Makamba akizungumza kabla ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani Dar es salaam, Agost 3, 2022.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) unaolenga kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo kwa kuwapatia mafunzo, maeneo ya mashamba, mitaji na kuwaunganisha na fursa za masoko.
“Vijana wetu fursa ni nyingi nchini kwetu, sekta ya kilimo inabeba fursa zaidi ya asilimia 50, kitendo cha wizara kuzindua mpango mkakati wa vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo ni mpango unaolenga kuboresha uchumi wa mto mmoja mmoja kuanzia umri wa vijana.”
Mheshimiwa Majaliwa amezindua mradi huo wa Program ya Ajira kwa Vijana kupitia Sekta ya Kilimo leo (Jumatano, Agosti 3, 2022) katika maonesho ya siku kuu ya wakulima Nane Nane yanayofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Pia, Waziri Mkuu amewataka vijana wachangamkie fursa zilizopo katika mradi huo ikiwa ni pamoja na kujihusisha na kilimo cha mazao mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Awali, Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde alisema programu hiyo itakayowahusisha vijana wa nchi nzima itaanzania na mkoa wa Dodoma na Mbeya kwa ajili ya majaribio na wametenga ekari 69,000.
Alisema maeneo hayo yataandaliwa na kusafishwa na Serikali kabla ya kuwapatia vijana. “Pia vijana watapatiwa pembejeo na kuweka mifumo mizuri ya umwagiliaji, lengo ni kutengeneza ajira zaidi ya milioni tatu.”








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...