Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge ametoa tahadhari kwa wananchi wa Pwani na Dar es Salaam kuwa waangalifu wa matumizi ya maji kutokana na hali ya upungufu.
Akizungumza na waandishi wa wa habari Kunenge amesema mwaka jana kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji hivyo mwaka huu hatutarajii kuwepo kwa upungufu wa maji kwani maji ni uhai na wananchi hivyo anatoa tahathari mapema ili kuondokana na uhaba wa maji kwa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.
"Ni wajibu wetu kama viongozi tuliopewa dhamana kusimamia Rasilimali zetu za maji zinalindwa vizuri na kutumika vizuri." Alisema Kunenge
Pia amesema kuwa kulingana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na taarifa za tahadhari za Mamlaka ya Hali ya Hewa inaonesha kipindi hiki hakutakuwa na mvua za kutosha hivyo inabidi kusimamia vyanzo vya maji ili kuweza kuondokana na upungufu wa maji kwenye Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam
"Tunapoona kiwango cha upatikanaji wa maji kinaendelea kutokuwa himilivu kulingana na mahitaji yetu ya kawaida kwa ajili ya kulinda uhai Dar Es Salaam kuanza kutumia maji kwa uhangalifu kwa kuacha kutumia maji hovyo kwa kuamini kuwa unaweza kulipa bili za maji." Alisema Kunenge
Pia ameushukuru uongozi wa Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira (DAWASA) pamoja na Bonde la Wami-Ruvu kwa kufuatilia kwa karibu hali ya maji hasa kwenye mto Ruvu.
"Nafahamu kuna baadhi ya Wananchi wameishapewa vibali vya kutumia maji kwa shughuli za kilimo na najua mmeishawapa taarifa ya kutoendeleza mashamba yao kwa sasa ili wasitumie maji kwenye shughuli ya kilimo kwa kipindi hiki." Alisema Kunenge
Kunenge amesema kuwa wale wote wenye vibali halali na bado wanaendelea kutumia maji kwa shughuli za kilimo wasitumie mara moja mpaka watakapopewa taarifa huku wakiangalia mwendendo mzima wa upatikanaji wa maji.
Amesisitiza kuwa wale wote ambao hawataki kuzingatia Sheria hasa wanaohujumu miundombinu ya maji, wizi, wanaotumia maji bila kufuata Sheria na taratibu na wale wote wanaoleta mifugo kwenye vyanzo vya maji kuacha mara moja.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tahadhari zinazobidi kuchukuliwa ili kusiwepo na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemejana kulia ni Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy
Baadhi ya wakurugenzj wa DAWASA pamoja na mfanyakazi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani wakifuatilia mkutano wa mkuu wa Mkoa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...