Na Mwandishi wetu

Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika Bara la Afrika na ya 12 duniani kuwa mwenyeji Mashindano ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani baada  ya mashindano hayo kufanyika mara 12 baada ya kuanzishwa kwake.

Kauli hiyo imetolewa  katika mkutano wa Waandishi wa Habari leo Oktoba 28,2022 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas na Rais wa Mashindano ya Urembo na Utanashati kwa Viziwi Duniani, Bonita Lee kutoka nchini Marekani.

Shindano hilo litafanyika kesho JNICC Dar ea Salaam ambapo Mhe Rais Samia Suluhu Hassan atawakilishwa na Mhe. Doroth Gwajima Waziri wa Jinsia,  Wanawake na Makundi maalum Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.   Mohamed Mchengerwa ambaye atakuwa mgeni maalum.

Dkt. Abbas amefafanua kuwa  Serikali imewapa  zawadi  washindi wote wa shindano hilo la kidunia  na  viongozi kutembelea mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro Oktoba 31,2022  baada ya kumalizika kwa shindano hilo kesho ikiwa ni mwendelezo wa Royal Tour  aliyoiasisi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amesema tukio hilo litarushwa  na mitandao  mbalimbali duniani  ikiwa na pamoja na kituo cha televisheni cha AZAM  ambacho kitarusha mbashara kupitia kipindi chake cha Sinema zet  kuanzia majira ya saa mbili usiku. 

Pia amesema  katika  tukio hili   maalum itawajumuisha  waalikwa zaidi ya 1000 ambapo filamu ya Royal Tour  iliyochezwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan itaanza kuonyeshwa  ili watu waweze jinsi Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na   vivutio mbalimbali vya utalii.

Aidha, ameongeza  kwamba   burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa  miziki mbalimbali zitaoneshwa  kwa washiriki na ameomba  washiriki kuwa tayari kupokea matokeo kutoka kwa majaji  kwani  hadi kufika  hapa tayari wote  ni washindi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wahabari leo Oktoba 28 Jijini Dar es salaam  mara baada ya kutangaza rasmi kilele cha fainali ya Shindano la dunia la utanashati,urembo na mitindo ambapo litafanyika rasmi kesho Oktoba 29 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam likihudhuriwa na viongozi mbalimbali

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbas akiwa na washiriki wa shindano la dunia la utanashati,urembo na mitindo Jijini Dar es salaam  mara baada ya kutangaza rasmi kilele cha fainali ya Shindano la dunia la utanashati,urembo na mitindo ambapo litafanyika rasmi kesho Oktoba 29 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam likihudhuriwa na viongozi mbalimbali
Rais wa Viziwi Afrika Habibu Mlope( aliyenyanyua mikono) akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es salaam kuelekea mashindano ya ya kidunia  Mister na Miss Kiziwi Oktoba 29 mwaka huu
Rais wa Dunia wa Viziwi Bonita Annleek ( katikati waliokaa) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari( hawapo pichani) kuhusu mashindano ya kidunia ya Mister na Miss Kiziwi ,kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya  Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...