
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
KIJANA Fabian Sebastian amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kuwadhalilisha marais wastaafu, Ally Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete kwa njia ya mtandao.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi Grace Mwanga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Evodia Kyaruzi na imedai mshtakiwa ametenda makosa hayo mwezi Septemba mwaka huu.
Wakili Mwanga amesema, Septemba 21 mwaka huu katika sehemu isiyofahamika kupitia akaunti ya Tick-tock iitwayo Fabylee mshtakiwa alichapisha picha ya Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi na kuandika 'ipi ingekuwa pisi kali'
Katika shitaka la pili imedaiwa kuwa, siku na mahali pasipojulikana, mshyakiwa huyo kupitia akaunti yake hiyo alichapisha picha ya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na kuandika ' ipi ingekuwa pisi kali'.
Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo ametakiwa na mahakama kuleta wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh. Milioni tatu.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 20 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...