WATUHUMIWA  40 wa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kuvunja nyumba usiku maarufu panya road wamefikishwa mahakama ya Wilaya ya Ilala Kinyerezi Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Jeshi la Polisi, Dar es Salaam 6 Oktoba 2022 Mahakama ya Wilaya ya Ilala Oktoba 5, 2022 imemsomea mashtaka Lubea Manzi maarufu Master, pamoja na wenzake 39 waliofikishwa mbele ya Mahakimu watatu, Hakimu Mkazi Glory Nkwera, Fadhili Luvinga, Rehema Liana, wakikabiliwa na mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kuvunja nyumba usiku na kujeruhi watu maeneo mbalimbali ya Wilaya, Ilala, Dar es Salaam.

Mwendesha mashtaka wakili wa serikali Michael Momboko, Magdalena Kisoka, Aziza Mhina walisema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo tarehe 19 -21/09/ 2022 maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam ambapo walivunja nyumba usiku na walipora mali baada ya kuwajeruhi wananchi kwa kutumia silaha za jadi (mapanga, nondo, visu) na kukimbia.

Watuhumiwa hao kwa pamoja walikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kutokana na mashataka wanayowakabiliwa nayo kutokuwa na dhamana.

Kesi hiyo imeaharishwa mpaka tarehe 19/10/2022 na upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...