Na Abel Paul-Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa ya mauaji ya watu watatu wakiwepo askari wawili wa Jeshi la Uhamiaji na mwananchi mmoja yaliyotokea katika kijiji cha Mtakuja, Kata ya Lulembela, Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita

Akitoa taarifa hiyo leo tarehe 26.10.2022 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishina msadizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi SACP DAVID MISIME amesema kuwa majua hayo yametokea muda wa 04:00 usiku wa kuamkia leo October 26.

Misime amewataja walio uawa katika tuki hilo ni  Mkaguzi wa Jeshi la Uhamiaji Salum Msongela Mpole na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Gilbert Edward, ambao wote kituo chao cha kazi ni  wilaya ya Bukombe.

Samabamba na hilo amemtaja Mwananchi aliyeuawa katika tukio hilo kuwa ni  Juma Bundala mkazi wa Kijiji cha Mtakuja. Pia amesema kuwa askari mmoja konstebo wa uhamiaji amejeruhiwa katika tukio hilo ambapo alikimbizwa hosptali kwa matibabu zaidi.

SACP Misime amesema kuwa chanzo cha tukio hilo la mauaji ni baada ya askari hao kufika katika kijiji hicho baada ya kupata taarifa za uwepo wa wahamiaji haramu katika nyumba ya mwananchi mmoja kijijini hapo amabapo amebainisha kuwa hadi sasa watu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na tukio hilo.

Amebainisha kuwa tayari Timu ya uchunguzi imeshatumwa kwenda katika kijiji hicho, kufanya uchunguzi wa mazingira yote yanayozunguka tukio hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa kulingana na ushahidi utakaokusanywa na timu hiyo.

Aidha Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Mtakuja kuwa watulivu na kufuata sheria wakati wa uchunguzi ukiendelea.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...