Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara kutoka kampuni hiyo, Oscar Kisanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2022 na kutambulisha Mfumo wenye kifaa kitakachorekodi makosa ya Madereva wa vifaa vya moto.
Mkuu wa Uperesheni usalama barabarani Makao Makuu ya Polisi na Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Adam Maro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, wakati Kampuni ya Cogsnet Technologies wakitoa maelekeze jinsi Mfumo wa vitronic jinsi utakavyofanya kazi barabarani.
Kifaa Kinachorekodi makosa ya madereva wa Vyombo vya moto
Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara kutoka kampuni hiyo, Oscar Kisanga akimwelezea Mkuu wa Uperesheni usalama barabarani Makao Makuu ya Polisi na Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Adam Maro namna Mfumo wenye kifaa cha kurekodi makosa ya madereva wa vifaa vya moto.

* Kurekodi kila kila Kosa linalofanyika, Madereva wajiandae
*Teknologia zaidi kutumika, Polisi  Usalama barabarani waona shangwe


KUTOKANA na Changamoto ya Ajali hapa nchini ambazo zinaondoa Maisha ya watu wengi mapema, Kampuni ya Cogsnet Technologies  imekuja na kifaa maalumu kwa ajili ya kupiga picha na kurekodi makosa ya Madereva wa magari barabarani.

Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara kutoka kampuni hiyo, Oscar Kisanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2022 amesem  teknolojia hiyo ambayo imeshaanza kutumika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki itapunguza ajali za barabarani.

Amesema kuwa teknolojia hiyo inaweza kuleta mapato kwa serikali kwani dereva anapofanya kosa barabarani lazima alipi pia itaongeza ajira kwa watanzania.

Akizungumzia kuhusiana na mfumo huo wa vitronic  unaotunza umeme kwa siku saba hadi nane amesema kuwa wapo katika majaribio ya kuonesha jinsi mfumo huo unavyofanya kazi na unavyoweza kutatua migogoro kati ya madereva na matrafiki barabarani.

 Amesema mfumo huo unachukua makosa katika nyanja tatu ambapo kama dereva ataendesha kwa spidi kubwa, atakayepita kwenye mataa yanayoonesha rangi nyekundu na Dereva akipita kwenye kwa kutanua.

"Makosa hayo yote yatakuwa captured na hii system ambayo itakuwa inawasiliana na data centre moja kwa moja kwa ajili ya kurekebisha makosa ya barabarani." Amesema Kisanga 

Amesema mfumo huo pia utakuwa umeunganisha na Leseni za madereva na mamba za vitambulisho vya Taifa (NIDA) na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ili kumbaini mtu aliyefanya kosa barabarani kwa kuonesha muda na eneo ambalo dereva amefanya kosa.

Kisanga ametolea  mfano kwa madereva wanaotembea kuanzia saa sita usiku hupita kwenye taa nyekundu kwa kuangalia huku na huku na kupita lakini sasa mfumo huo wa kieletroniki utawabaini na kuwakatia tiketi ya kosa lake na kutakiwa kulipia faini.

Amesema kuwa Jeshi la polisi usalama barabarani watatakiwa kwenda kwenye kituo cha taarifa ili waweze kuwabaini wale ambao wamepigwa faini na hawajalipia kulingana na sheria za jeshi la polisi usalama barabarani.

Ameongeza kuwa mfumo huo pia utawafunza watanzania kuwa na nidhamu barabarani kwani nchi nyingi duniani zimefanikiwa kwa kutumia mfumo huo. "Mfumo huu utachukua Makosa yote yanayofanywa na Mabasi, magari madogo, bajaji na pikipiki." Amesema Kisanga


Mkuu wa Uperesheni usalama barabarani Makao Makuu ya Polisi na Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Adam Maro amesema teknolojia hiyo imechelewa kuja nchini ndio maana serikali inaharaka kufanya utafiti na kuimarisha barabara nchini ili kuweza kupata mfumo huo ili taarifa za makosa ya ajali za barabarani. 

Katika majaribio yaliyofanyika ufukwe wa Coco leo kwa muda mchache amasema kuwa makosa yaliyopatikana ni makosa zaidi ya 417 ambayo ni changamoto kukamatwa na Trafiki wa Usalama barabarani kwa macho ya Kawaida.

"Tunaamini hii ni mwarobaini kabisa kwa sababu magari yameongezeka, unakuta dereva amelikurupusha gari kama amekatwa kichwa  haangalii kama kunawatumiaji wengine wa barabara kwa hiyo Mwarobaini wao ndio huu hapa."

Amesema anaamini kuwa watalazimika kubadilika na ile ya kusema "Askari alinipiga tochi amenionea mfumo huo hautamwonea mtu kwa sababu ikishasetiwa basi kinachokuwa kinasomeka hapo ndio ushahidi ambao unaweza kupelekwa hata mahakamani."

Vilevile amesema mfumo huo unaweza kupambana na majambazi ambao wanapora simu au Mkoba karibu na Mataa barabarani kwani utakuwa unarekodi na kupiga picha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...