Kuwepo kwa Kitita cha Huduma za Afya Nchini Kutasaidia Serikali kuweza kuwahudumia kikamilifu Wananchi wake.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa Kauli hiyo katika Hotuba iliyosomwa kwa Niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Hafla ya Uzinduzi wa Kitita cha Huduma za Afya uliofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar .

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya pamoja na kusimamia Kitita hicho imejipanga kufanya mageuzi makubwa kuhakikisha Fedha kwa ajili ya kuboresha         Huduma za Afya zinapatikana kikamilifu.

Ameeleza kuwa Mageuzi hayo ni pamoja na kuanzishwa kwa Huduma ya Bima ya Afya ambayo inategemewa kuanza kufanya kazi miezi michache ijayo pamoja na kutafuta vyanzo mbadala vya fedha.

Aidha Rais Dkt Mwinyi ameutaka Uongozi wa Wizara ya Afya kusimamia utekelezaji wa Kitita hicho yanafikiwa na kuhakikisha Mifumo ya Taarifa pamoja na ufuatiliaji na tathmini ipo Imara.

Amesema ni Wajibu kwa Wizara ya Afya kusimamia utekelezaji wa Kitita hicho kwa mashirikiano na Wizara na Taasisi mbali mbali ili kufikia malengo ya kuwepo kwa Kitita hicho.

"Ili tuweze kufikia malengo, nasisitiza kuwepo ushirikiano wa karibu zaidi baina ya Taasisi pamoja na Wadau wote watakohusika kwa njia moja ama nyengine"

Sambamba na hayo wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Serikali itaendelea kupitia Vipaumbele vya Sekta ya Afya na kujipanga upya kutokana na Mazingira ya sasa inayosababishwa na ongezeko la Idadi ya Watu.

 "Kufuatia ongezeko la Idadi ya watu pamoja na Mabadiliko ya Kiuchumi, Serikali imejikuta ikilazimika kupitia tena vipaumbele vyake na kujipanga upya kutokana na mazingira ya sasa"

Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ameeleza kuwa Lengo la kuandaliwa kwa Kitita hicho ni Kusaidia Wananchi wa Zanzibar kupata Huduma sawa za Afya kwa Vituo vyote vya Afya Mijini na Vijijini pasi na  kuwepo utofauti wowote.

Aidha ameeleza kuwa kitita hicho kitasaidia kuongeza ufanisi kwa watoa Huduma ya Afya Nchini hasa kuzingatia kuongezeka kwa Idadi ya Wananchi hapa Zanzibar.

Nae Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bwana Max Mapunda ameeleza kuwa Shirika hilo limeridhishwa na kitita hicho na kuongeza kuwa WHO itaendelea kutoa mashirikiano katika utekelezaji wa Kitita hicho ili kufikia malengo ya kuboresha Huduma za Afya Zanzibar.

Akielezea Muhtasari wa Kitita hicho Dkt. Omar Mwalim ameeleza kuwa Kitita hicho kinaeleza Wizara  kujua Maradhi yanachukua nafasi kubwa nchini pamoja na kujua namna ya kujikinga juu ya maradhi yasiyoambukiza

 

Wakuu wa Taasisi na Mashirika mbali mbali ndani na nje ya Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akihutubia kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika hafla ya Uzinduzi wa Kitita cha Huduma za Afya Hafla iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege.
Dkt. Omar Mwalim akieleza kwa Muhtasari yaliyokuwemo katika Kitita cha Huduma za Afya kwenye Hafla ya uzinduzi wa kitita hicho iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mzrui akieleza machache katika Hafla ya uzinduzi wa Kitita cha Huduma za Afya iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza katika Hafla ya uzinduzi wa Kitita cha Huduma za Afya Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege zanzibar.

  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...