NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi amefanya ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kuendeleza utalii kupitia Fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Akiwa katika hifadhi hiyo Naibu Katibu Mkuu Juma Mkomi amekagua ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara ,madaraja, viwanja vya ndege na maeneo ya maegesho ya ndege za watalii uliofanyika katika hifadhi hiyo.
Amesema kukamilika kwa miundombinu hiyo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ni kichocheo kikubwa cha kuinua shughuli utalii na kuifanya hifadhi hiyo iendelee kupata idadi kubwa ya watalii wa ndani na nje ya nchi ambao wamekua na mchango mkubwa katika uchumi na maendeleo ya Taifa.
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire inasifika duniani kwa kuwa makundi makubwa na mengi ya Tembo nchini Tanzania. Pia ina mandhari nzuri ya kuvutia inayotokana na maumbile ya mibuyu mikubwa, wanyamapori wa aina mbalimbali wakiwemo pundamilia, nyumbu, swala, simba, nyati, kongoni, chui, duma na aina mbalimbali za dege ambao wanaopatikana ndani ya hifadhi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...