Madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa akiongea wakati wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa juu ya utovu wa nidham kwa watumishi wa serikali

Diwani wa viti maalum tarafa ya Idodi Wilayani Iringa Shani Msambusi akitoa taarifa juu ya mhudumu huyo wa afya juu ya utendaji wake wa kazi

Diwani wa kata ya Kising'a Ritha Mlagala akichagia hoja wakati wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa





Na Fredy Mgunda, Iringa.

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Iringa Limeagiza kufanyika uchunguzi wa haraka dhidi ya Mhudumu wa afya katika Zahanati ya Kijiji ya Tungamalenga, anayedaiwa kutumia singano iliyotumika kumtibu mgonjwa

Akizungumza wakati wa baraza la Madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa alitoa agizo kwa Idara ya afya baada ya hoja ya malalamiko dhidi ya Mhudumu huyo wa afya anayedaiwa kukiuka misingi ya utumishi akijihusisha na vitendo vya utovu wa nidham ikiwemo ulevi wa kupindukia nyakati za kazi.

Mhapa alisema Halmashauri hiyo haitovumilia utovu wa nidham unaopelekea ukiukwaji mkubwa wa misingi ya kitaaluma na kuhatarisha afya za wagonjwa wanaopata huduma katika zahanati hiyo kwani kitendo cha kutumia sindano iliyotumika kumtibu mgonjwa mwingine kinaweza kusababisha kusambaa kwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo maambukizi ya virusi vya ukimwi

"Tumeagiza uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo kwenye zahanati zote na Mimi kama mwenyekiti napenda kutoa onyo kwa watumishi wote wa Halmashauri hii ninataka kupata taarifa kamili katika Baraza la madiwani lijalo ili tushughulike na hao watendaji"alisema Mhapa

Aliyasema hayo baada ya Diwani wa viti maalum tarafa ya Idodi Wilayani Iringa Shani Msambusi kuwasilisha malalamiko hayo katika baraza la madiwani na kumtaja mhudumu huyo wa afya aliyefahamika kwa jina la Johavina Mjuni kuwa ni kero kwa wananchi wanaopata huduma katika zahanati hiyo kutokana na utovu wa nidham uliokithiri na kushindwa kufanya kazi kwa weledi.

Diwani Msambusi alilielezabaraza la Madiwani kuwa Wananchi wanaiomba Serikali kuchukua hatua kwani hawako tayari kuendelea kuhudumiwa na Mhudumu huyo na kusisitiza Serikali kumuhamisha kwa kuwa hawana imani tena na huduma za kiafya anazozitoa.

Msambusi alisema kuwa mhudumu huyo wa afya amekuwa anatumia vilevi kupitiliza kipindi cha kazi hadi kushindwa kufanya kazi kwa weledi wake wa kuhudumia wananchi wagonjwa.

Kufuatia malalamiko hayo Kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,Luvanda Witson alisema wanaanzisha uchunguzi wa haraka dhidi ya madai hayo na pindi watakapojiridhisha hatua za kinidham zitachukuliwa na kulijulisha baraza la madiwani kuhusu hatua hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...