WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema anafurahishwa na mafanikio makubwa ya utekelezwaji wa ujenzi miradi mbalimbali ya maendeleo yanayoonekana katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

“Wana-Ruangwa lazima tuendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Haya ni mafanikio makubwa, Ruangwa kwa maendeleo inawezekana.”

Amesema hayo leo (Jumatano, Februari 22, 2022) baada ya kukagua ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa (Ruangwa Girls) pamoja na madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kitandi wilayani Ruangwa.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anaridhia kutoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali ya utoaji huduma za jamii hapa nchini hivyo ni jukumu la kila wananchi ni kuitunza ili ilete faida anayoikusudia

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanafunzi kwamba wajitahidi kufanya vizuri kwenye masomo yao “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameweka mkazo katika elimu, ambayo inatolewa bure kuanzia awali hadi kidato cha sita”

Naye Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telak amewataka wazazi wawape watoto nafasi ya kushiriki kikamilifu katika masomo ili waweze kutimiza ndoto zao


“Jitahidini kufanya vizuri kitaaluma, mjitambue nyie ni wanafunzi na hivyo mjiepushe na vishawishi vyovyote vitakavyokwamisha maendeleo yenu kitaaluma. Wananchi tuwalinde watoto wetu ili watimize ndoto zao. Mtoto wa mwenzio ni wako.”

Pia, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuacha kuvamia maeneo ya karibu kwa kuwa Serikali imeyahifadhi kwa ajili matumizi ya baadae ya taasisi husika. “Hapa palikuwa pori hapakuwa na shamba pasiguswe.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa madarasa ya ghorofa yanayojengwa katika shule ya msingi Likangara, ambapo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa ubunifu wa mradi huo. Mradi huo unahusisha vyumba vinane vya madarasa, matundu 24 ya vyoo na ofisini nne.




waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama michoro ya Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasicha Ruangwa wakati alipokagua mradi huo, Februari 22, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, February 22, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua chumba cha maabara katika shule mpya ya Sekondari Kitandi iliyopo Ruangwa, Lindi Februari 22, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wakazi wa eneo la kitandi, Ruangwa, Lindi wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari Kitandi, Februari 22, 2023.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...