MKUU wa Wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu ametembelea vyombo vya habari vilivyopo Wilayani Rungwe na kujionea vipindi mbalimbali vinavyorushwa vituo hivyo sambamba na kuzungumza na wananchi.
Vituo alivyotembelea ni pamoja na redio Rungwe na Chai FM vyote vikiwa Tukuyu Mjini na akiwa kwenye vituo hivyo ambavyo amevitwmbelea nyakati tofauti amesema hivyo yombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali.
Akieleza zaidi Hainiu ambaye kitaaluma ni muandishi wa habari mwenye uzoefu mkubwa ameeleza wazi kuwa hlvyombo hivyo havina budi kuandaa vipindi vitakavyoelimisha jamii, kuhamasisha, kuikosoa na kuburudisha jamii.
"Vombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuhamasisha watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule kufanya hivyo mapema ili kuwawezesha kupata haki yao ya Msingi kwa Maendeleo na Ustawi wa taifa la Tanzania."
Haniu amesema kwamba Tanzania kupitia Mradi wa Boost imeanza kuboresha miundombinu ya kutolea huduma ya elimu ya Msingi ambapo Ujuzi kwa walimu, Vitabu, Vyoo na madarasa yatajengwa.
Akizungumzia Sekta ya kilimo, Mkuu wa Wilaya Haniu amesema Serikali imeendelea kusambaza bolea ya ruzuku kwa wakulima wilayani Rungwe na kuonya mawakala pamoja na wakulima wanaouza na kununua mbolea hiyo kwa njia ya udanganyifu kuacha kufanya hivyo kwani wanarudisha nyuma juhudi za Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuwaletea Maendeleo wananchi Wake.
Pia amesema Serikali imeendelea kuboresha masoko ya bidhaa mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo ( Wamachinga) ili kutoa fursa ya kujiongezea kipato Cha kila siku.
" Wananchi niwambie, unapojengewa soko maana yake kumsaidia mteja ajue bidhaa ipi ataipata wapi. Vivyo hivyo wamachinga, soko la ndizi na bidhaa zingine Masoko haya yamesaidia sana likiwemo soko la Mwambenja lililofunguliwa leo"
Haniu ameagiza wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika maeneo yaliyotengwa kwa nia nzuri ya kuboresha mandhari ya mji, Usafi wa mazingira, Mapato ya Serikali na Usalama wa Mali zao.
Katika hatua nyingine Haniu ameagiza wakazi wa Wilaya ya Rungwe kuacha migogoro ya ardhi na kuwa imekuwa ikihatarisha amani na utulivu katika Jamii.
Amesema Ofisi yake pamoja na Mabaraza ya ardhi amekuwa akitatua migogoro mbalimbali ya ardhi sambamba na utoaji elimu dhidi ya Matumizi bora ya ardhi na kuandika Wosia kwa ngazi ya kaya hali itakayomaliza migogoro hiyo katika Wilaya ya Rungwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...