Wakazi wa kanda ya mikoa ya kaskazini ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro wamekoshwa baada ya bia ya KIBO GOLD kurudi tena baada ya kukosekana kwa kipindi cha miaka 5 sokoni.

Kurudi tena kwa bia hii inalenga kudumisha historia ya kipekee kwa SBL kutengeneza bia yenye kilele cha ladha ileile bora na adimu ambapo pia chapa hii imeshuhudiwa kunyakua tuzo mbalimbali za dhahabu kama ya Monde Section kwenye mashindano yaliyofanyika mjini Bordeaux, nchini Ufaransa mwaka 2014.

Bia ya KIBO GOLD sasa inarejea ikiwa na mwonekano maridadi kwa kutengenezwa kwa ubora usio na kifani – ikiwa na viungo vya asilia na kutokuwa na sukari ya ziada na kwa bei ya 1,500/- tu.

Akizungumza katika uzinduzi wa bia hio mwanzoni mwa wiki hii mjini Moshi, Meneja Uvumbuzi wa SBL, Bertha Vedastus, alisema, ‘’Kama SBL tunalenga kupanua wigo wetu wa bidhaa kuhakikisha tunakidhi mahitaji ya wateja wetu popote walipo. Na kama tunavyojua Watanzania tunathamini sana urithi na utamaduni katika kila jambo tunalolifanya. 

Hivyobasi, tunapotafuta maendeleo katika maisha yetu ya kila siku, ni muhimu kuhifadhi na kuthamini urithi na utamaduni wetu. Na kwayo, uwepo wetu wa muda mrefu katika kanda ya Kaskazini umetufanya kuja na maamuzi ya kina ya kudumisha urithi na ufahari wa kanda hii kupitia bia ya KIBO GOLD.

Bertha aliendelea kuelezea kuwa bia ya KIBO GOLD ina utajiri wa kihistoria na urithi wa ubora ambao kila mtanzania inabidi ajivunie kuuendeleza. Alinukuliwa, ‘ni bia yetu, ya watu wetu na urithi wetu. Tunaamini KIBO GOLD - Kilele Cha Ubora, itaendelea kuwa chaguo la kwanza kwa wapenda bia katika kanda hii nzima’’.

SBL baada ya kutambua mara moja uwezo na thamani ya chapa hiyo ya KIBO GOLD imedhamiria kuirejesha katika mioyo ya wapendwa wa bia kote Ukanda wa Kaskazini. Bia hii yenye sura mpya ya kisasa kwa bia itaongeza mvuto wake kwa soko la ndani na la nje.

Mkurugenzi wa Masoko na Uvumbuzi SBL, Anitha Rwehumbiza (wa pili kulia) akitangaza kurejea kwa Bia ya KIBO GOLD. Wa pili kushoto ni Meneja Uvumbuzi SBL, Bertha Vedastus, wa kwanza kushoto akiwa ni Mkurugenzi wa Biashara SBL, Chris Gitau na wa kwanza kulia ni Meneja Mauzo kanda ya kaskazini, Patrick Kisaka.

Meneja Uvumbuzi kutoka SBL, Bertha Vedastus (watatu kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika tukio la kutangaza kuirudisha tena bia ya KIBO GOLD kanda ya kaskazini. Wa kwanza kulia ni Meneja Chapa Uvumbuzi, Joseph Innocent, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uvumbuzi, Anitha Rwehumbiza. Wa kwanza kushoto ni Meneja Masoko kanda ya kaskazini, Andrew Msiagi, wa pili kushoto ni Meneja Mauzo kanda ya kaskazini, Patrick Kisaka na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara, Chris Gitau. 


Mkurugenzi wa Masoko na Uvumbuzi, Anitha Rwehumbiza akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari.

Viongozi wa SBL wakitoa ishara ya kutangaza rasmi kurejea kileleni kwa bia ya KIBO GOLD 


Wafanyabiashara mbalimbali wakiburudika na bia hio wakati katika hafla hio iliyofanyika mjini Moshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...