*Afunguka A_Z yaliyomkuta London

Na.Khadija Seif, Michuzi Blog

MSANII wa muziki wa bongo fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ambaye pia ni balozi wa kampuni ya michezo ya kubahatisha, WinPrincess amefunguka jinsi kampuni hiyo ilivyomsaidia kurudia Tanzania mara baada ya kukwama nchini London alipokua akifanya show licha ya yeye kuwa Balozi wa Kampuni hiyo.

Gigy Money ameongea hayo Leo July 25,2023 katika uzinduzi wa namba mpya ya kituo cha msaada wa michezo ya kubashiri ya kampuni ya Winprincess iliofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Nimekuwa nikijisikia fahari na kujivunia kuwa Balozi wa Makampuni mbalimbali lakini kwa Kampuni ya kubeti ya "Winprincess" nimekuwa nikicheza michezo ya kubahatisha kupata laki nane, fedha hiyo nikaeda kulipia ada ya mtoto wangu" pamoja na Kampuni hiyo Kunipatia tiketi ya kurudi nchini Tanzania mara baada ya kukwama nchini London wakati wa show yangu kusitishwa ."

Nae Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hakan Aric, amesema huduma hiyo waliyozindua wateja watapiga bure kwa lengo la kupata msaada.

"Kutokana na mchezo huu wa kubahatisha kushika kashika kasi na wateja wengi kuongeza katika kampuni ya Winprincess hivyo tumetangaza rasmi namba itakayowawezesha wateja wetu kufikiwa kwa urahisi katika kupata huduma za kubashiri."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...