-Huduma ya Free Wi-fi kupatikana viwanja vya maonesho ya Sabasaba, TanzaKwanza yapongezwa kwa ubunifu
SERIKALI imedhamiria kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kidigitali kwa kufanya mapitio ya sera, mikakati na sheria ili ziendane na Tanzania ya kidigitali kama dunia inavyoenda ili Taifa linufaike kiuchumi kupitia digitali.
Hayo yameeelezwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa jukwaa la TEHAMA lililoratibiwa na kampuni ya TanzaKwanza kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE,) katika maonesho maonesho ya 47 ya Biashara Tanzania 'Sabasaba' hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa huduma ya mtandao (Free Wi-fi) katika viwanja hivyo vya maonesho.
Waziri Nape amesema, moja ya hatua ya kuelekea uchumi wa kidigitali ni pamoja na jitihada za ujenzi wa miundombinu ikiwemo anwani za makazi, minara ya Mawasiliano na mkongo waTaifa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita.
"Nimeelekeza anwani za makazi zianzie hapa Sabasaba ili kila anayetembelea maonesho haya aelekezwe na vibao vya anwani......minara ya Mawasiliano na mkongo waTaifa inafika kila mahali itarahisisha utoaji huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao zikiwemo huduma za mahakama, mikutano na huduma za afya na hiyo ni pamoja na sera, sheria na miundombinu madhubuti ni dhahiri tutafikia uchumi wa kidigitali." Amesema.
Pia ameipongeza Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) kwa kushirikiana na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) kwa kufanikisha kuleta huduma ya mtandao Free Wi-fi katika viwanja hivyo vya maonesho hali itakayokuza biashara ya Tanzania.
Aidha amesema wataendelea kushirikiana na nchi mbalimbali ikiwemo Malawi katika kukuza sekta ya TEHAMA pamoja na kuongeza huduma zaidi za kimtandao za Kimataifa kwa watanzania.
Awali Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaKwanza ambao ndio waandaji wa jukwaa hilo Tumaini Magila amesema, lengo la jukwaa hilo ni kuleta pamoja wadau kutoka Serikalini na taasisi binafsi kupitia majadiliano yenye tija na kukuza sekta ya TEHAMA.
"77 Expo Village ni jukwaa la kwanza katika maonesho haya na limelenga kuleta pamoja sekta 8 za kimkakati kwa kuanzia ili kujadili fursa zilizopo pamoja na changamoto na mwisho kutoka na suluhu kwa manufaa ya Taifa kama Serikali ya awamu ya sita inayoongizwa na Rais Samia Suluhu Hassan ilivyodhamiria." Amesema.
Magila amesema kuwa, katika maonesho hayo jukwaa la 77 Expo Village limefanikiwa kwa asilimia 75 na wataendelea kuboresha zaidi hususani kuwakutanisha wadau kutoka Serikalini na taasisi binafsi ili kuboresha zaidi sekta za kimkakati ikiwemo Madini, Nishati, Uchukuzi, Kilimo na TEHAMA.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE,) Latifa Khamis amesema Mamlaka hiyo haipo nyuma katika matumizi ya TEHAMA na kwa mwaka huu wametumia mifumo mbalimbali kwa njia ya mtandao ikiwemo mifumo ya malipo, mfumo wa tiketi ambao umefanikiwa kwa asilimia 95, mfumo wa malipo, vitambulisho vya ushiriki pamoja na ugawaji mabanda kwa washiriki hususani washiriki kutoka nje ya nchi ambavyo vilifanyika kwa njia ya mtandao.
Vilevile Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Selestine Kakele ameipongeza kampuni ya TanzaKwanza kwa ubunifu na kuandaa jukwaa hilo muhimu ambalo wananchi wamepata fursa ya kufahamu nini Serikali inafanya katika kuboresha sekta hiyo pamoja na kupokea maoni kutoka kwa wadau ili kuboresha zaidi.
Ni mara ya kwanza maonesho ya Biashara Tanzania 'Sabasaba' kuwa na jukwaa la majadiliano "77 Expo Village ' ambapo Wizara na taasisi zilizo chini yake wamekutana na kuonesha bidhaa, rasilimali watu na huduma wanazotoa pamoja na kujadili fursa na changamoto katika maboresho zaidi kwa manufaa ya Taifa.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa la TEHAMA '77 Expo Village ' na kueleza kuwa mapitio ya sera, mikakati na sheria itaifikisha Tanzania katika uchumi wa kidigitali. Leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi. Kundo Mathew akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa hilo na kueleza kuwa kupongeza jitihada za Serikali katika kuwahudumia watanzania katika sekta ya TEHAMA. Leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Selestine Kakele akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa hilo na kueleza kupongeza ubunifu wa kampuni ya TanzaKwanza kwa kukutanisha Wizara na Taasisi zake kwa lengo la kujadili fursa na changamoto. Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Latifa Khamis akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa hilo na kueleza kuwa Mamlaka hiyo haipo nyuma katika matumizi ya TEHAMA hususani katika mifumo ya kutoa huduma, Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaKwanza Tumaini Magila akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa hilo na kueleza kuwa wataendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kupita jukwaa hilo ambalo kwa mwaka huu wamefanikiwa kwa asilimia 75, Leo jijini Dar es Salaam.

Matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa jukwaa la TEHAMA.
SERIKALI imedhamiria kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kidigitali kwa kufanya mapitio ya sera, mikakati na sheria ili ziendane na Tanzania ya kidigitali kama dunia inavyoenda ili Taifa linufaike kiuchumi kupitia digitali.
Hayo yameeelezwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa jukwaa la TEHAMA lililoratibiwa na kampuni ya TanzaKwanza kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE,) katika maonesho maonesho ya 47 ya Biashara Tanzania 'Sabasaba' hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa huduma ya mtandao (Free Wi-fi) katika viwanja hivyo vya maonesho.
Waziri Nape amesema, moja ya hatua ya kuelekea uchumi wa kidigitali ni pamoja na jitihada za ujenzi wa miundombinu ikiwemo anwani za makazi, minara ya Mawasiliano na mkongo waTaifa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita.
"Nimeelekeza anwani za makazi zianzie hapa Sabasaba ili kila anayetembelea maonesho haya aelekezwe na vibao vya anwani......minara ya Mawasiliano na mkongo waTaifa inafika kila mahali itarahisisha utoaji huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao zikiwemo huduma za mahakama, mikutano na huduma za afya na hiyo ni pamoja na sera, sheria na miundombinu madhubuti ni dhahiri tutafikia uchumi wa kidigitali." Amesema.
Pia ameipongeza Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) kwa kushirikiana na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) kwa kufanikisha kuleta huduma ya mtandao Free Wi-fi katika viwanja hivyo vya maonesho hali itakayokuza biashara ya Tanzania.
Aidha amesema wataendelea kushirikiana na nchi mbalimbali ikiwemo Malawi katika kukuza sekta ya TEHAMA pamoja na kuongeza huduma zaidi za kimtandao za Kimataifa kwa watanzania.
Awali Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaKwanza ambao ndio waandaji wa jukwaa hilo Tumaini Magila amesema, lengo la jukwaa hilo ni kuleta pamoja wadau kutoka Serikalini na taasisi binafsi kupitia majadiliano yenye tija na kukuza sekta ya TEHAMA.
"77 Expo Village ni jukwaa la kwanza katika maonesho haya na limelenga kuleta pamoja sekta 8 za kimkakati kwa kuanzia ili kujadili fursa zilizopo pamoja na changamoto na mwisho kutoka na suluhu kwa manufaa ya Taifa kama Serikali ya awamu ya sita inayoongizwa na Rais Samia Suluhu Hassan ilivyodhamiria." Amesema.
Magila amesema kuwa, katika maonesho hayo jukwaa la 77 Expo Village limefanikiwa kwa asilimia 75 na wataendelea kuboresha zaidi hususani kuwakutanisha wadau kutoka Serikalini na taasisi binafsi ili kuboresha zaidi sekta za kimkakati ikiwemo Madini, Nishati, Uchukuzi, Kilimo na TEHAMA.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE,) Latifa Khamis amesema Mamlaka hiyo haipo nyuma katika matumizi ya TEHAMA na kwa mwaka huu wametumia mifumo mbalimbali kwa njia ya mtandao ikiwemo mifumo ya malipo, mfumo wa tiketi ambao umefanikiwa kwa asilimia 95, mfumo wa malipo, vitambulisho vya ushiriki pamoja na ugawaji mabanda kwa washiriki hususani washiriki kutoka nje ya nchi ambavyo vilifanyika kwa njia ya mtandao.
Vilevile Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Selestine Kakele ameipongeza kampuni ya TanzaKwanza kwa ubunifu na kuandaa jukwaa hilo muhimu ambalo wananchi wamepata fursa ya kufahamu nini Serikali inafanya katika kuboresha sekta hiyo pamoja na kupokea maoni kutoka kwa wadau ili kuboresha zaidi.
Ni mara ya kwanza maonesho ya Biashara Tanzania 'Sabasaba' kuwa na jukwaa la majadiliano "77 Expo Village ' ambapo Wizara na taasisi zilizo chini yake wamekutana na kuonesha bidhaa, rasilimali watu na huduma wanazotoa pamoja na kujadili fursa na changamoto katika maboresho zaidi kwa manufaa ya Taifa.

Matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa jukwaa la TEHAMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...