Na Brown Jonas WUSM Dar Es Salaam

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana leo Agosti 12, 2023 Jijini Dar es Salaam amewahimiza washairi kutumia Sanaa hiyo kutunga mashairi yatakayosaidia kukemea mmomonyoko wa maadili nchini.

Mhe. Chana amesema hayo katika kilele cha Kongamano la tatu la Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA)

“Hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili
hasa vijana na watoto kupuuza mila na desturi za kitanzania kwa kuiga tamaduni za kigeni. Ushairi ni mojawapo ya nyenzo ya kukemea vitendo vinavyokiuka maadili yetu na kuelimisha jamii kuthamini misingi ya utamaduni wetu.” amesema Dkt. Chana

Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sanaa za ushariki kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambapo kongamano la Nne limepangwa kufanyika Jijini Dodoma mapema mwakani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...